Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Baba yetu alitutupa sasa Amefariki ,tunataka kumsamehe tufanyaje?


SWALI

 

assalam alaykum warahmatuh-llah wabarakatuh.

swala langu ni kuhusu babayangu, Aliyefariki kwanzia afariki sijawahi kumuombea mungu kwa sababu nilikuwa na uchungu sana wa kuwa hakuweza kutuangalia kwa lolote kwanzia kuzaliwa kwangu, na hata ndugu zangu.  Yaani ametutupa kwa kila kitu,kwahivyo hatukuwa na uhusiano hata kidogo twajua tu yule ndio baba yetu, kila nikikaa najiuliza kwa nini ametufanya hivi na alikuwa akijiweza hata kututazama alikuwa hakutaka tu!  Mpaka sasa ndio naona nimeanza kurudi nyuma manake nisingelipenda kumchukia mpaka ikafika hali ya zaidi ningelipenda kumuombea dua anisamehe na vile ashafariki mungu amsamehe. tafadha kwa kila shukrani munisaidie manake yananisumbua sana.ahsante.

 

 

JIBU

Waleykum Salaam WarahmatulLaah Wabarakatuh
 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hapana shaka kutokana na hisia zako ulizokuwa nazo kuhusu aliyefariki mzazi wako kuwa zimetokana na hali ilivyokuwa baina yenu na aliyefariki mzazi wenu ambaye hakuwa akikutazameni. Lakini tunapenda kukumbusha kwamba vyovyote itakavyokuwa yeye ni mzazi wako, na pia hamuwezi kujua sababu gani alifanya hivyo. Kwa hiyo mpeni udhuru kwa kumdhania vizuri badala ya kumwekea dhana mbaya kama inavyopasa baina wa Waislamu. Juu ya hivyo kwa vile ni mzazi wako hakuna budi kumuombea kwani ni maamrisho kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala).

 

Kumsamehe makosa yake na kumuombe du’aa mzazi wenu kutapatikana faida kubwa kuliko kuzidi kuweka chuki. Kwani kwa vyovyote imeshatokea la kutokea na ima uchague kumuombea du’aa na kumfanyia wema ambao utaendelea kumfikia na kumnufaisha, au umwache aendelee kuteseka mzazi wako huko katika maisha yake ya Barzakh nawe huku ubakie na dukuduku, huzuni na dhiki? Ipi mojawapo itakayokupa wewe furaha? Bila ya shaka kumsamehe na kumfanyia wema!  Faida zenyewe ni zifuatazo:

 

1. Utakuwa umetekeleza amri za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) za kuwaombea du’aa mzazi au wazazi wako.

 

2. Kila utakapomuombea Maghfirah atakuwa anapandishwa daraja moja juu, na hali itakuwa kama ilivyo katika usimulizi ufuatao:

 

 

عن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : قال رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْه ِ وَ سَلَّمَ : إِنَّ الرَّجُلَ لَتُرْفَعُ دَرَجَتُهُ فِي الْجَنَّةِ   فَيَقُولُ : أَنَّى هَذَا ؟ فَيُقَالُ :باسْتِغْفَارِ  وَلَدِكَ لَكَ))لإمام أحمد  و في سنن ابن ماجة أيضاً بإسنادٍ صحيح  

 

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mtu hupandishwa daraja yake Peponi. Kisha huuliza: Kwa ajili ya nini? [huku kupandishwa kwangu daraja?] Huambiwa: Kwa ajili ya kuombewa Maghfirah na mtoto wako)) [Ahmad, na katika Sunan Ibn Maajah ikiwa na isnaad Swahiyh]

 

3. Kumsamehe mtu ni sawa na kusamehewa wewe madhambi yako. Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipotaka kumgomea kuendelea kumsadiia jamaa yake ambaye alikuwa mmojawapo aliyechangia katika uzushi wa kumzulia mwanawe  Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhaa), Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akateremsha Aayah ifautayo:

 

((وَلاَ يَأْتَلِ أُوْلُوا الْفَضْلِ مِنْكُمْ وَالسَّعَةِ أَنْ يُؤْتُوا أُوْلِي الْقُرْبَى وَالْمَسَاكِينَ  وَالْمُهَاجِرِينَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلْيَعْفُوا  وَلْيَصْفَحُوا أَلاَ تُحِبُّونَ أَنْ يَغْفِرَ اللَّهُ لَكُمْ  وَاللَّهُ غَفُور ٌ رَحِيم))

((Na wala wasiape wale wenye fadhila miongoni mwenu na wenye wasaa wa mali kuwa hawatowapa (swadaqah) jamaa wa karibu, na masikini, na Muhaajiriyn katika njia ya Allaah. Na wasamehe na waachilie mbali. Je, hampendi Allaah Akughufurieni? Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu)) [An-Nuwr: 22]

 

Hisia zako tayari zinaonyesha kuwa unakaribia kumsamehe na hii ni alama ya iymaan na mapenzi ya kimaumbile baina ya mtoto na mzazi. Kwa hiyo usiache Shaytwaan akakughilibu na kukubakisha katika hali isiyomridhisha Mola wako Mtukufu wala kukuridhisha wewe nafsi yako. Muombee mzazi wako Maghfirah, muombee du’aa na mfanyie wema kama kwamba yuhai duniani.

 

Na la muhimu zaidi ni kuwa uwape nasaha ndugu zako wote nao wapate ujumbe huu na nyote mtapata malipo mema kutoka kwa Mola wenu.

 

Na Allaah anajua zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...