Ruka hadi kwenye maudhui makuu

al-Fawzaan akielezea rai tatu tofauti za Ahl-us-Sunnah kuhusu darsa na mawaidha ya video na kwenye TV

Swali: Inajuzu kurekodi kanda za mihadhara kwa njia ya video na kuuza kanda hizi katika baadhi ya maduka ya rekodi? Pamoja na kuzingatia ya kwamba kunakuwepo vilvile kanda za maonyesho na tamthiliya/filamu zinazoitwa “tamthiliya/filamu za Kiislamu”. Ni yepi maoni yako juu ya hilo?

Jibu: Masuala ya kurekodi mihadhara kwa njia ya video au kwa njia ya TV ni jambo ni jambo limefanyiwa utafiti. Upande mmoja ndani yake kuna manufaa; kuwafikishia watu kheri na kuwafundisha. Lakini upande mwingine kuna madhara vilevile; picha. Kwa hivyo masuala haya ni yenye mashaka. Iwapo tutatazama zile kheri zinazopatikana ndani yake tunaweza kusema kwamba kheri inatakiwa kuenezwa. Lakini tukitazama picha zinazopatikana ndani yake tunaweza kusema kuwa haya ni madhara na wala haijuzu kuchukulia wepesi suala la picha ambalo limeharamishwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hiyo jambo hili mimi nimenyamaza. Kutokana na ninavyojua wanachuoni wana maoni tatu:

1- Wapo ambao wanaonelea kuwa ni haramu. Wameupa nguvu upande wa uharamu kutokana na jambo la picha. Hawa wanaonelea kuwa kuna uwezekano wa kuwafunza watu na kueneza elimu pasi na kutumia njia hii.

2- Wapo wengine ambao wameupa nguvu upande wa manufaa na wakajuzisha kurekodi mihadhara ya kidini ya video na kwenye TV kwa kutazama zaidi upande wa manufaa. Wanachuoni hao wao wenyewe wameshiriki na kuhudhuria kwenye TV. Wapo wanachuoni waliofanya hivi. Wana mtazamo wao unaoangaliwa.

3- Kuna wengine ambao wamenyamaza.

Kwa hivyo masuala kuna utafiti ndani yake. Kila mwanafunzi ayape nguvu yale maoni ambayo anaonelea yeye kuwa yana nguvu. Kuhusu mimi nanyamaza kuhusu masuala haya.

Kuhusu filamu hakuna tamthiliya/filamu za Kiislamu. Tamthiliya/filamu hizi ni za maonyesho. Kwa hiyo zinatakiwa kuitwa “tamthiliya/filamu za maonyesho”. Vilevile zinatakiwa kuitwa “sanaa za kiaina”. Kusema kwamba ni tamthiliya/filamu za Kiislamu si kweli. Katika Uislamu hakuna tamthiliya/filamu kwa sampuli hii ambazo zimetuingilia kutoka huko Ulaya na Marekani. Uislamu umejitosheleza kutokamana na tamthiliya/filamu hizi.

Rejea https://soundcloud.com/user-621373875/al-fawzaan-kuhusu-mawaidha-ya-video-camera-na-kwenye-tv

Mhusika Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...