Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Filamu na Anaashiyd kwenye vituo vya majira ya joto

Filamu na Anaashiyd kwenye vituo vya majira ya joto

Swali 2: Kwenye majira ya joto kunachezwa filamu na Anaashiyd. Ni yapi maoni yako juu ya hilo?


Jibu: Ni wajibu kwa wasimamizi wa vituo vya majira ya joto kusitisha vitu vyote visivyokuwa na faida au vyenye madhara kwa wanafunzi. Wawafunze Qur-aan, Sunnah, Hadiyth, Fiqh na lugha ya kiarabu. Yanatosheleza na kwa kule kuchukua wakati. Wanatakiwa kuwafunza pia elimu ambayo itakuja kuwanufaisha katika dunia kama mfano wa kuandika, hesabu na ujuzi wenye faida. Mambo yanayoitwa “burudani” hayatakiwi kuwepo kwenye barnamiji[1]. Yanapoteza wakati. Pengine hata yakawasumbua na lile lengo lililowaleta. Miongoni mwa mambo hayo ni filamu na Anaashiyd. Haya si jengine isipokuwa ni pumbazo na mchezo. Ukiongezea juu ya hilo yanawafanya wanafunzi kuangalia michezo ya kuigiza na kusikiliza muziki unaorushwa kwenye vyombo vya khabari.

[1] Shaykh Swaalih al-Fawzaan amesema:

“Kitu ambacho inatakikana kukisisitiza ni yale ambayo vijana wengi wenye dini wametumbukia ndani yake. Wanasikiliza Anaashiyd zinazoimbwa kwa sauti za pamoja na wanaziita kuwa ni “Anaashiyd za Kiislamu”. Ni aina ya nyimbo na wakati mwingine zinaimbwa kwa sauti zenye kufitinisha. Mikanda hii inauzwa pamoja na mikanda ya Qur-aan na mihadhara ya dini. Anaashiyd hizi kuziita kuwa ni “Anaashiyd za dini” ni makosa. Kwa sababu Uislamu haukutuwekea Anaashiyd. Kinyume chake umetuwekea kumdhukuru Allaah, kusoma Qur-aan, kujifunza elimu yenye manufaa na kadhalika.

Kuhusiana na Anaashiyd ni katika dini ya Suufiyyah iliyozushwa. Wameifanya dini kuwa ni pumbazo na mchezo. Kuzifanya Anaashiyd ni katika dini ni jambo limeshabihiana na manaswara ambao dini yao wameifanya nyimbo na sauti za pamoja.

Lililo la wajibu ni kutahadhari na Anaashiyd hizi na kupiga marufuku kuuzwa na kusambazwa. Isitoshe Anaashiyd hizi zinaweza kuchochea katika hamasa zenye fitina na uchochezi kati ya waislamu.

Wanaeneza Anaashiyd hizi kwa kutumia hoja ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaweza kusomewa mashairi na akasikiliza na kuzikubali. Jibu ya hilo ni kwamba mashairi yaliyokuwa yakisomwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayakuwa yanasomwa kwa sauti za pamoja kwa sampuli ya nyimbo. Vilevile hayakuwa yanaitwa “ya Kiislamu”. Ilikuwa ni mashairi ya kiarabu yaliyo ndani yake na hekima, methali, ujasiri na ukarimu. Maswahabah walikuwa kila mmoja akiyasoma kivyake kutokana na maana yaliyokuwa nayo. Walikuwa wanaweza kusoma mashairi wakati wanapofanya kazi za nguvu kama ya ujenzi au safari za usiku. Ni dalili inayoonyesha kuwa yameruhusiwa mambo kama hayo katika hali kama hizo, sio kuyafanya kuwa ni somo katika kulea na kufanya Da´wah, kama inavyofanya leo pindi wanafunzi wanapojifunza Anaashiyd hizi na kuziita kuwa ni “Anaashiyd za Kiislamu” au “Anaashiyd za kidini”. Hii ni Bid´ah katika dini na zinatoka katika dini ya Suufiyyah iliyozushwa. Wao ndio wenye kujulikana kufanya Anaashiyd kuwa ni kipengele cha dini.

Ni wajibu kuzindua kampeni hizi na kupiga marufuku kuuzwa mikanda hii. Shari huanza ikiwa ndogo. Ikiwa mtu hazisimamishi mapema zitakuja kuendelea na kukua.” (al-Khutab al-Minbariyyah (03/184-185)

Muheshimiwa Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn aliulizwa kuhusu Anaashiyd za Kiislamu. Hapa chini kunafuatia swali na jibu:

Swali: Je, inajuzu kwa wanaume kuimba Anaashiyd za Kiislamu? Je, inajuzu kuwapigia dugu wanapoimba? Je, inajuzu kuimba Anaashiyd mbali na sikukuu na sherehe?

Jibu: Anaashiyd za Kiislamu ni Anaashiyd zilizozushwa. Zimeshabihiana na waliyozusha Suufiyyah. Kwa hivyo inatakiwa kwa mtu kujitenga nazo mbali kwa mawaidha katika Qur-aan na Sunnah. Isipokuwa tu labda katika vita ili ziweze kusaidia kuleta motisha na Jihaad katika njia ya Allaah (Ta´ala). Ni vizuri. Anaashiyd zikifuatanishiwa na dufu zinakuwa bado ziko mbali kabisa na usawa. (Fataawaa ash-Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn (01/134-135))


  • Marejeo: al-Adjwibah al-Mufiydah ´an As'ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 20-22

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...