Swali: Ni ipi hukumu ya kuchukua mihadhara na semina kwa kutumia kifaa cha video camera?
Jibu: Naona kuwa hakuna ubaya kurekodi mihadhara na semina kwa kifaa cha video camera haja ikipelekea kufanya hivo au manufaa yakapelekea kufanya hivo kutokana na yafuatayo:
La kwanza: Kurekodi ambako ni moja kwa moja (live) hakuingii katika kuiga uumbaji wa Allaah. Hilo liko wazi kwa wale wenye kuzingatia.
La pili: Picha haionekani kwenye mkanda. Kwa hivyo hakuna kitendo cha kuhifadhi picha.
La tatu: Tofauti iliyopo ya kuingia video camera katika kuiga uumbaji wa Allaah – hata kama hilo linarithisha kufanana – hakika haja au manufaa yaliyohakikiwa hayafanyi tofauti kuisha katika jambo ambalo haijabaini namna ya kukatazwa kwake.
Rejea Majmuu´-ul-Fataawaa (02/284)
Mfasiri Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Maoni