Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kutoa Zakaatul-Fitwr Kwa Kiwango Zaidi Ya Anachostahiki Maskini Na Kutoa Siku Kumi Kabla Ya Ramadhwaan Kumalizika

SWALI:

Assalam alaykum,

naomba kuuliza,

1. _*ikiwa mie natakiwa kutoa Zakaatul fitr yenye thamani ya pesa zaidi ya laki moja na nayelenga kumpa ana hitajio la juu sana, yajuzu kumpatia zaka iyo siku 10 kabla ya Eid el fitr?*_

 

2. _*je naweza kumpatia kiasi cha zaidi ya ile ninayowajibikiwa kutoa nikiwa na niya ya kumfanya awapendezeshe watu wa nyumbani kwake na awalishe pia?*_
 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Wa 'Alaykumus Salaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh,

 

Zakaatul-Fitwr hutolewa chakula na si pesa kwa mujibu wa Ahaadiyth zilizopokelewa katika mlango huo.

 

Dalili:

 

Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma) amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliifanya kutoa swaa' (pishi) ya tende au swaa' (pishi) ya shayiri (ngano) kuwa ni Zakaatul-Fitwr iliyowajibika kwa Waislamu wote, mtumwa aliye huru, mwanamke na mwanamume, kijana na mzee, na akaamrisha kwamba itolewe kabla ya watu kwenda kuswali (Swalaatul-'Iyd). [Al-Bukhaariy]

 

Abu Sa'iydil-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Tulikuwa tukilipa Zakaatul-Fitwr swaa' (pishi) moja ya chakula, au swaa' (pishi) ya shayiri (ambacho ndicho kilichokuwa chakula chao zama hizo) au swaa' (pishi) ya tende au swaa' (pishi) ya aqit (mtindi mkavu) au swaa' (pishi) ya zabibu" [Al-Bukhaariy]

 

 

Kwa dalili hizo, ni dhahiri kwamba Zakaatul-Fitwr lazima iwe ni chakula, si pesa. Hivyo lazima tutekeleze ilivyoamrishwa katika Sunnah. Hivyo lipa swaa' (pishi) moja ya chakula chochote kinachotumika na watu katika nchi yako mfano mchele au ngano kwa ajili yako na kila mtu katika nyumba yako. (swaa' (pishi) ni sawa na taqriban kilo 2 na nusu au kilo 3).

 

 

Kwa hiyo, ikiwa pesa zake atazitoa ili zinunuliwe aina ya hiyo ya chakula kinacholiwa zaidi hapo mjini kwake kama vile mchele, basi hakuna neno kama hizo pesa zitanunuliwa mchele na kisha kugaiwa kwa wanaostahiki.

 

Muda wa kuitoa kwa kauli sahihi ambayo Wanachuoni wameenda nayo kwa mujibu wa baadhi ya mapokezi, ni kutolewa Zakaatul-Fitwr jua linaposhuka siku ya mwisho wa Ramadhwaan au Alfajiri ya siku ya 'Iyd kabla ya Swalaah ya 'Iyd kwa sababu ndio wakati wake na ndio lengo lake.

 

Ingawa kuna ikhtilaaf na kauli nyingi kuhusu suala hilo la muda wa kuitoa na kuna waliosema inaweza kutolewa hata mwanzo wa Ramadhwaan na wengine walioona inaweza kutolewa masiku kabla na wengine siku moja au mbili kabla kwa mapokezi yafuatayo:

 

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu anhuma) ambaye amesema: Walikuwa wakitoa Zakaat al-Fitwr siku moja au mbili kabla (Ya 'Iyd). [Al-Bukhaariy].

 

 

Ama kuhusu kutoa ziada kwa maskini kwa ajili ya kumtimizia mambo yake mengine na kumpa furaha na familia yake, hilo halikatazwi kwa mujibu wa Ahlul-'Ilm.

Isipokuwa kama wapo maskini wengine na hawajapata Zakaatul-Fitwr, ni bora kutanguliza kuwapatia wao ili waifurahie sikukuu yao kuliko kumpa ziada mmoja.

 

Na Allaah Anajua zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...