*Swali*
Asalam alaykum, shekh :mm nna mchumba angu lkn anakua mgumu kuja kuleta posa nymbani, jee? nimsomee dua gani ili aweze Kuja haraka maana ni cku nyingi tena naomba unisaidie unifahamishe ustadh.
*Majibu*
Wa Aleykum Sallaam WarahmatulLaah Wabarakatuh
BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa Ba’ad.
*Maana ya Uchumba Kisheria*
✅Uchumba katika Uislamu ni pale *mwanamme anayetaka kuoa au jamaa zake au mtu yeyote aliyemwakilisha anapokwenda kwa wazazi wa msichana/Bint/Mwanamke* kuposa/kupeleka Barua na kukubaliwa.
*✅Huo ndio unaitwa uchumba*
➡Ama kinyume na hivyo unakuwa ni urafiki baina ya mvulana na msichana. *Na hili katika Uislamu limekatazwa kwani ni Haramu*
✅Na hili limekatazwa kishari’ah.
➡Na hapo katika Swali lako umesema kwamba una Mchumba wako Lakini anakuwa mgumu *kuleta posa nyumbani* ina maana kuwa Huyo mwanaume *Kisheria si Mchumba wako kwasababu bado hajapeleka barua ya Posa nyumbani kwenu*
➡Katika Uislamu Hakuna *Boyfriend wala Girlfriend* na hii ni *Haramu*
➡Ayaah na dalili za kukataza jambo hili zipo nyingi zikiwa zinazoashiria makatazo moja kwa moja (directly) na nyinginezo zenye uhusiano na makatazo haya.
➡Kuwa na boyfriend bila shaka kutasababisha yatendeke maasi baina ya mwanamke na mwanamume kwani shaytwaan huwa pamoja nao akiwachochea kuingia katika kumuasi Mola wao⤵
عن عمر رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم : ((ما خلا رجل بامرأة إلا كان الشيطان ثالثهما)) الترمذي
Kutoka kwa 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hachanganyiki mwanamume na mwanamke ila shaytwaan huwa ni watatu wao))
↪Imepokelewa na Imaam At-Tirmidhiy
✅Ndio maana pia Mtume Muhammad ((Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameonya kukaa faraagha mwanamke na mwanamume⤵
قال صلىالله عليه سلم : ((لا يخلوّنّ أحدكم بامرأةإلا مع ذى محرم)) متفق عليه
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hawi faraagha mmoja wenu pamoja na mwanamke ila awepo Mahram wake))
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy Na Muslim
➡Matokeo yake ni shaytwaan kuwafikisha kuingia katika maasi ya zinaa na ndio maana sheria ya Kiislamu haikuruhusu jambo hilo au kufunga uchumba inavyojulikana engagement. Bali inatakiwa kufunga ndoa moja kwa moja baada ya kuwafikiana pande zote.
➡Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)⤵
((وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَأُوتُواْ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّمُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلاَ مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ وَمَنيَكْفُرْ بِالإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَالْخَاسِرِين))
((Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa waliopewa Kitabu kabla yenu, mtakapowapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anayekataa kuamini bila shaka amali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara))
↪Surat Al-Maaidah Aya ya 5
✅Hizo ni mila za kikafiri ambazo zinapasa tuepukano nazo na ambazo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametuonya⤵
((وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُم))
((Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao))
↪Surat Al-Baqarah Aya ya 120
✅Ewe Msichana wa Kiislamu unapokabiliwa na mvulana kutaka kufanya urafiki ujiepushe kabisa bali umshauri kwanza awasiliane na wazazi wako na baada ya kumjua kuwa ni mtu mwenye dini na tabia nzuri basi wazazi wasichelewa kukuozesha nawe uridhike kwani hivyo ndivyo ipasavyo na tulivyopewa mafunzo kutoka kwa Mtume Muhammad(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam⤵
((إِذَا خَطَبَ إِلَيْكُمْمَنْ تَرْضَوْنَ دِينَهُ وَخُلُقَهُ فَزَوِّجُوهُ إِلَّا تَفْعَلُوا تَكُنْ فِتْنَةٌفِي الْأَرْضِ وَفَسَادٌ عَرِيضٌ)) رواهالترمذي وقال الألباني : حسن
((Atakapoposa kwenu yule mtakaeridhika na dini yake, na tabia yake, basi muozesheni, kwani kutokufanya hivyo itakuwa fitna katika ardhi (duniani) na ufisadi mpana (mkubwa) ))
↪Imepokelewa na Imaam At-Tirmidhiy kasimulia na Shaykh Albaaniy amesema ni Hadiyth Hasan.
*Ewe Mwanamke akitokea Mwanaume anayetaka kukuoa kabla hujamkubalia kwenda kupeleka Barua ua Posa nyumbani kwenu Tafadhali Swali Swalah ya Istikhaarah*
✅Istikhaarah maana yake ni kuomba uchaguzi au aumuzi katika jambo.
➡Na Swalah ya Istikhaarah hakika ni zawadi kubwa tuliyopewa sisi Umma wa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم, kwani ina faida kubwa sana kwetu kwani hatuamui jambo letu tunaloliomba katika Swalah hii, ila baada ya kumuomba Allaah سبحانه وتعالى Atuamulie Yeye hilo jambo kama lina kheri na sisi Atufanikishe nalo na kama ni la shari Atuepushe nalo.
➡Yeye Pekee Allaah سبحانه وتعالى Ndiye mwenye kujua ya ghayb (yasiyoonekana) yaani yatakayotokea siku za mbele yaliyokuwa yameshandikwa katika Lawhun Mahfuudhw.
*Na Dua ya Kuomba katika Swalah ya Istikhaarah ilivyokuja katika Du'aa kuwa tunasema⤵*
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْتَخيـرُكَ بِعِاْـمِك، وَأسْتَقْـدِرُكَ بِقُـدْرَتِـك، وَأَسْـألُـكَ مِنْ فَضْـلِكَ العَظـيم، فَإِنَّـكَ تَقْـدِرُ وَلا أَقْـدِر، وَتَـعْلَـمُ وَلا أَعْلَـم، وَأَنْـتَ عَلاّمُ الغُـيوب، اللّهُـمَّ إِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ (وَيُسَـمِّي حاجته) خَـيْرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، ( عَاجِلِهِ و آجِلِه) فَاقْـدُرْهُ لي وَيَسِّـرْهُ لي ثـمَّ بارِكْ لي فيـه، وَإِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ شَـرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، ( عَاجِلِهِ و آجِلِه) فَاصْرِفْـهُ عَنّيِ وَاصْرِفْني عَنْـهُ وَاقْـدُرْ ليَ الخَـيْرَ حَيْـثُ كانَ ثُـمَّ أَرْضِـني بِِـه .
*"Allahumma inniy astakhiyruka bi’ilmika, wa astaqdiruka biqudratika wa as-aluka min fadhwlikal-‘adhwiym, fainnaka Taqdiru wa laa aqdir, wa Ta’alamu wa laa a’alamu wa Anta ‘Allaamul-ghuyuub. Allahumma in Kunta Ta’alamu anna haadhal-amra (Utaje jambo lako) Khayrul-liy fiy diyniy wa ma’aashiy, wa ‘aaqibati amriy, ‘aajilihi wa aajilihi Faqdir-hu-liy wa Yassirhu-liy, thumma Baarik-liy fiyh. Wain Kunta Ta’alamu anna haadhal-amra sharrul-liy fiy diyniy wa ma’aashiy wa ‘aaqibati amriy ‘aajilihi wa aajilihi, Faswrif-hu ‘anniy Waswrifniy ‘anhu Waqdir-liyal-khayra haythu kaana Thummar-dhwiniy bih"*
“Ewe Allah, hakika mimi nakutaka ushauri (muelekezo) kwa ujuzi Wako, na nakuomba Uniwezeshe kwa uwezo Wako, na nakuomba fadhila Zako kubwa, hakika Wewe Unaweza, nami siwezi, nawe Unajua nami sijui, nawe ni Mjuzi wa yale yaliyofichikana. Ewe Allah, iwapo jambo hili kutokana na ujuzi Wako (utalitaja jambo lako) lina kheri na mimi katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (karibu na mbali) basi nakuomba Uniwezeshe nilipate, na Unifanyie wepesi, kisha Unibariki, na iwapo unajua kwamba jambo hili ni shari kangu katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (karibu na mbali) basi Liepushe na mimi na Niepushe nalo, na Nipangie jambo jengine lenye kheri nami popote lilipo, kisha Niridhishe kwalo”
✅Kwa hiyo inampasa Muislamu awe anaitumia sana Swalah hii kwa kila jambo lake, likiwa ni dogo au kubwa kwani juu ya kupata faida ya kwamba unamuachia Allaah سبحانه وتعالى Mwenye Ujuzi Mwenye Hikma kutuamulia, pia unapata thawabu za kuswali Raka'ah mbili.
✅Lakini haifai kuswali Swalah hii kwa ajili ya mambo maovu au anapotaka mtu kutimiza fardhi.
➡Mfano mwizi haimpasi kuiswali Swalah hii ili atake uamuzi kama akaibe au la maana kuna baadhi ya Waumini hawachelewi kuniuliza maswali . Au mwanamke asiiswali Swalah hii ikiwa yuko katika wasiwasi wa shaytwaani unaotaka kumpelekea kufanya zinaa na kadhalika.
⏩Vile vile asiswali mtu Swalah hii katika kutimiza mambo ya kheri kama mfano kutimiza fardhi ya kutoa Zakah au Sadaka na kadhalika wakati shaytwaan atakapokutia wasiwasi kukuzuia kutenda amali hizo njema.
✅Swalah hii inaweza kutumika katika mambo yanayofaa mfano unataka kwenda safari, au umeomba kazi katika shirika fulani, au unataka kuoa au mwanamke amekuja kuposwa na kadhalika.
Na Allaah anajua zaidi
Imeandaliwa na *Manhaj Salafy Mtwara*
Maoni