Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tashahhud inayofaa

*Katika Tashahhud inafaa Kusema “Assalaamu ‘Alaan Nabbiy” Badala ya Kusema “Assalaamu ‘Alayka Ayyuhan Nabbiy”..?*

✅Naam,  Inaonekana kulingana na swali lako hukumuelewa vizuri huyo ndugu aliyekuambiwa hayo kwani katika Tashahhud hakuna kusema *Swallu 'alan Nabiy*. Hakuna riwaya hata ya kutungwa ambayo inatueleza hilo.

➡Hata hivyo, inaonyesha kuwa katika kuandika au kusikia ima ulisikia au uliandika makosa badala ya Assalaamu 'alan Nabiy ukasikia au ukaandika Swallu 'alan Nabiy.

➡Hili tamko ambalo umeliandika mara nyingi hutumiwa na baadhi ya watu katika mihadhara na mawaidha wakitaka kuwarudisha watu katika kusikiliza mawaidha kwa kusema Swallu 'alan Nabiy, ingawa haya ni mambo yasiyothibiti na yasiyo na dalili. Kwa hiyo, tutajaribu kukuelezea kwa mujibu wa haya marekebisho ambayo tumeyafanya ili kuwe na faida kwa wasomi wa tovuti hii yenu.

✅Uislamu  kama ulivyo umewekewa vitu sahali na vyepesi kwa maslahi yetu sisi binadamu. Jambo hili humfanya kila mwanadamu anayefuata nidhamu hii kuweza kutekeleza maagizo bila kuchoka wala kuona shida. Kwa ajili hiyo ndio Allaah Aliyetukuka Akatuambia⤵

'Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini' (22: 78).
Na tena:

'Allaah Anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito'
↪Surat Al-Baqarah Aya ya  185.

⏩Na kuhusu sifa kemkemu alizokuwa nazo Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam), Allaah Aliyetukuka Anasema: '… anawaamrisha mema na anawakataza yaliyo mabaya, na kuwahalalishia vizuri na kuwaharimishia vibaya, na kuwaondolea mizigo yao na minyonyoro iliyokuwa juu yao' (7: 157). Mizigo hii ni ile sheria ngumu waliokuwa Mayahudi wameamriwa kufuata.

⏩Kwa minajili hiyo, Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) akawa anawafundisha Maswahaba zake na hivyo kutufundisha sisi hasa katika duaa na adhkaar nyingi katika jambo moja ili iwe rahisi kwetu kufuata.

➡Ikiwa Muislamu ameshindwa kuhifadhi du’aa moja ambayo ni ngumu au ndefu basi kwa jambo lile zipo sahali na fupi kwake kuweza kuhifadhi.

⏩Ama tukija katika Tashahhud kama vile katika rukuu au sijdah utapata adhkaar nyingi kwa maslahi yake.

⏩Muislamu atachagua katika zile zilizo sahihi apendayo kuisoma ili atimize Ibaadah yake kwa njia iliyo nzuri yenye kuafikiana na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam).

➡Hebu tuzitazame baadhi ya Tashahhud alizofundisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)⤵

🅰Tashahhud ya Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu): Amesema alinifundisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Tashahhud kama alivyonifundisha Surah katika Qur-aan⤵

*At-tahiyaatu Lillahi wasw-Swalawaatu watw-Twayyibaatu as-Salaamu 'alayka ayyuhan Nabiyy wa Rahmatu Llaahi wa Barakaatuhu …..*(hii ni alipokuwa kati yetu, pindi alipoaga dunia tulisema: As-Salaamu 'alan Nabiy) [al-Bukhaariy, Muslim, Ibn Abi Shaybah na Abu Ya'laa).

⏩Na kauli hii ya Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu): Tulisema, as-Salaamu 'alan Nabiy, hii ilikuwa kwa kukubaliwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nayo inatiliwa nguvu na Hadiyth ya mama wa waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)
↪Muhammad Naaswir ad-Diyn al-Albaaniy, Swifatusw Swalaatin Nabiyy, uk. 161.

✅Kauli ya Tashahhud aina hii pia imepokewa kwa 'Umar bin al-Khatwtwaab (Radhiya Allaahu 'anhu) kama ilivyonukuliwa na Maalik na al-Bayhaqiy kwa Isnadi iliyo Sahihi na pia mama wa waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kama ilivyonukuliwa na Ibn Abi Shaybah na al-Bayhaqiy mbali na kwamba ipo tofauti kidogo katika baadhi ya maneno yaliyomo ndani yake.

🅱Tashahhud ya Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma)⤵

Amesema alikuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) akitufundisha Tashahhud kama alivyokuwa akitufundisha Surah katika Qur-aan. Alikuwa akisema⤵

*At-tahiyaatu al-Mubaarakatu asw-Swalawaatu atw-Twayyibaatu Lillaahi as-Salaamu 'alayka ayyuhan Nabiyy wa Rahmatu Llaahi wa Barakaatuhu ..…*
↪Imepokelewa na Imaam Muslim, Abu 'Awaanah, ash-Shaafi'iy na an-Nasaa'iy.

✅Tashahhud kama hii imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma) kama ilivyo katika Abu Daawuud na ad-Daraqutwniy, naye akaisahihisha. Pia Abu Muusaa al-Ash'ariy (Radhiya Allaahu 'anhu) amepokea kama hivyo kama ilivyonukuliwa na Muslim, Abu 'Awaanah, Abu Daawuud na Ibn Maajah.

⏩Hata hivyo Tashahhud walizofundishwa na Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) zimetofautiana baadhi ya lafdhi.

✅Kwa muhtasari ni kuwa Tashahhud utakayoitumia katika hizo utakuwa umesibu kufuata Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hivyo kuzidisha ujira wako na thawabu.

Na Allaah Anajua zaidi

Imeandaliwa na *Manhaj Salafy Mtwara*

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...