Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Fanya Ibadah kwa Wakati

*Fanya Ibadah kwa Wakati, Usipuuze*

✅Allaah (Subhaana wa Talaa) katika Surat An-Nisaa Aya ya 103 Anasema kwamba⤵

فَإِذَا قَضَيْتُمُ الصَّلَاةَ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ ۚ فَإِذَا اطْمَأْنَنتُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۚ إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا

Mtakapomaliza Swalaah, mdhukuruni Allaah msimamapo, na mkaapo na mnapolala ubavuni mwenu Mtakapopata utulivu, simamisheni Swalaah (kama desturi), hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu.

➡Maamrisho ya kutimiza Swalaah kwa wakati wake, na makemeo ya kuipuuza yamesisitizwa katika Qur-aan ana Sunnah na miongoni mwa Hadiyth za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni⤵

✅‘Abdullaah bin Mas'uwd  (رضي الله عنه)  amehadithia kwamba: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): Ni ‘amali gani inayopendeza kwa Allaah? Akajibu: “Ni kuswali kwa wakati wake.” Nikamuuliza tena: Kisha ni ‘amali gani? Akajibu: “Ni kuwafanyia ihsani wazazi.” Nikamuuliza tena: Kisha ni ‘amali gani? Akajibu: “Ni kupigana jihaad katika njia ya Allaah.”
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy Na Muslim.

✅Amesema pia: “Kitu cha kwanza atakachohesabiwa nacho mja Siku ya Qiyaamah katika ‘amali zake ni Swalaah, ikitengenea atakuwa amefuzu na amefanikiwa, na ikiharibika atakuwa ameshapita patupu na amekhasirika…”
↪Imepokelewa na Imaam At-Tirmidhy na amesema Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh.

✅'Abdullaah bin 'Amru bin Al-‘Aasw (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)   siku moja alitaja kuhusu Swalaah akasema: “Atakayeihifadhi atakuwa na Nuru na burhaan, na ataokoka Siku ya Qiyaamah, na asiyeihifadhi hatokuwa na Nuru wala burhaan wala hatookoka na Siku ya Qiyaamah atakuwa pamoja na Qaaruwn, Fir'awn, Haamaan na ‘Ubayy bin Khalaf))
↪Musnad Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh na amesema Al-Albaaniy Isnaad yake Hasan (Ath-Thamar Al-Mustatwaab (uk. 53).

✅Buraydah bin Al-Haswiyb  (رضي الله عنه)amehadithia kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akisema: “Mafungamano baina yetu na baina yao (wasio Waislamu) ni Swalaah, atakayeiacha atakuwa amekufuru.”
↪Imepokelewa na Imaam Ahmad, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah.

✅Imaam ibn Baaz (رحمه الله)  amesema: “Yeyote atakayeweka kengele ya saa makusudi imuamshe baada ya kutoka jua akakosa Swalaah ya Alfajiri, basi mtu huyo amepuuza kuswali kwa wakati wake na hivyo ni kufru kubwa kama walivyokubaliana ‘Ulamaa wengi kwa sababu amekusudia kuswali baada ya jua kutoka. Ni sawa na mtu ambaye anachelewesha kuswali Alfajiri akaiswali karibu na Adhuhuri.
↪Rejea Fataawa Ibn Baaz, Kitaab As-Swalaah 10/374

Na Allaah anajua zaidi

Imeandaliwa na *Manhaj Salafy Mtwara*

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...