Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Du'aa za Qunut ni Lazima zisomwe katika Swalah ya Alfajiri?

Swali

swali langu ni kwamba dua hii ya Qunut ni lazima iombwe usiku baa ya kusali rakaa mbili au unaweza ukaomba wakati wowote?
Pia naomba unipatie dua yenyewekama iko tofauti na ile isomwayo katika swala ya alfajir.

Jibu
BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa  aalihi waAswhaabihil Kiraamwa Ba’ad:
Kwanza tujue kwamba maana ya 'witr' (witiri) ni namba isiyoweza kugawanyika kama moja au tatu au tano na kadhalika. 
Na Swalah ya Witr ambayo ni Sunnah iliyosisitizwa sana, huswaliwa usiku baada ya Swalah ya 'Ishaa hadi asubuhi kabla ya Alfajiri. 
Hivyo hakuna Raka'ah mbili zinazoswaliwa usiku na kusomwa du'aa ya Qunuut kama ulivyosema, bali husomwa du'aa hiyo baada ya kuinuka kutoka kurukuu katika Raka'ah ya mwisho ya Swalah za Witr. 
Unaweza kuswali Raka'a tatu au tano au saba au tisa au kumi na moja. 
Utaswali Raka'a mbili mbili na kila baada ya Raka'a mbili utatoa salaam kisha utamalizia na Raka'ah moja ndio utasoma hiyo du'aa ya Qunuut baada ya kuinuka kutoka kurukuu. 
Na kama huna uwezo wa kuswali hivyo basi hata Raka'ah moja itakutosheleza kupata fadhila za Witr na kusoma du'aa ya Qunuut kutokana na dalili ya Hadiyth ifuatayo:   
((صلاة الليل مثنى مثنى فإذا خشيت الصبح أوتر بواحدة))أخرجه البخاري
((Swalah ya usiku ni (raka’ah) mbili mbili na ukiogopa kukukuta asubuhi  basi Swali Witr  [Raka'ah] moja)) [ Al-Bukhaariy]

Du'aa za Qunuut zilizothibiti katikaSunnah ni hizi zifuatazo unaweza kusoma moja wapo au zote.
اللّهُـمَّ اهْـدِنـي فـيمَنْ هَـدَيْـت، وَعـافِنـي فـيمَنْ عافَـيْت، وَتَوَلَّـني فيمَنْ تَوَلَّـيْت ، وَبارِكْ لـي فـيما أَعْطَـيْت، وَقِـني شَرَّ ما قَضَـيْت، فَإِنَّـكَ تَقْـضي وَلا يُقْـضى عَلَـيْك ، إِنَّـهُ لا يَـذِلُّ مَنْ والَـيْت، [ وَلا يَعِـزُّ مَن عـادَيْت ]، تَبـارَكْـتَ رَبَّـنا وَتَعـالَـيْت.
Allaahummah-diniy fiy man Hadayta, wa 'Aafiniy fiy man 'Aafayta, wa Tawallaniy fiy man Tawallayta, wa Baarik-liy fiy maa A'attawyta, wa Qiniy sharra maa Qadhwayta, Fainnaka Taqdhwiy  wa laa Yuqdhwa 'Alayka, innahu la yadhillu maw-Waalayta, wa laa ya'izzu man 'Aadayta, Tabaarakta Rabbanaa wa Ta'aalayta.
“Ee Allaah! Niongoze pamoja na Uliowaongoza, na Unipe afya njema pamoja na Uliowapa afya njema, na Nifanye kuwa ni mpenzi Wako pamoja na Uliowafanya  wapenzi na Nibariki katika Ulichonipa na Nikinge na shari ya Ulilolihukumu kwani Wewe Unahukumu wala Huhukumiwi. Hakika hadhaliliki Uliyemfanya mpenzi (wala hatukuki Uliyemfanya adui) Umetakasika Ee Mola wetu na Umetukuka"
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِرِضـاكَ مِنْ  سَخَطِـك، وَبِمُعـافاتِـكَ مِنْ عُقوبَـتِك، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْـك، لا أُحْصـي ثَنـاءً عَلَـيْك، أَنْـتَ كَمـا أَثْنَـيْتَ عَلـى نَفْسـِك
Allaahuuma inniy a'udhu Biridhwaaka min Swakhatwika, wa Bimu'aafaatika min 'Uquubatika, wa a'uudhu Bika Minka, laa ukhswiy Thanaan 'Alayka, Anta kamaa Athnayta 'Alaa Nafsika.
 “Ee Allaah! Hakika mimi najilinda kwa radhi Zako kutokana na hasira Zako na kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako, na najilinda  Kwako kutokana na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa Zako kwa kadiri ya idadi yake, Wewe ni kama Ulivyojisifu Mwenyewe”
اللّهُـمَّ إِيّـاكَ نعْـبُدْ، وَلَـكَ نُصَلّـي وَنَسْـجُد، وَإِلَـيْكَ نَسْـعى وَنَحْـفِد، نَـرْجو رَحْمَـتَك، وَنَخْشـى عَـذابَك، إِنَّ عَـذابَكَ بالكـافرين ملْحَـق. اللّهُـمَّ إِنّا نَسْتَعـينُكَ وَنَسْتَـغْفِرُك، وَنُثْـنـي عَلَـيْك الخَـيْرَ، وَلا نَكْـفُرُك، وَنُـؤْمِنُ بِك، وَنَخْـضَعُ لَكَ وَنَخْـلَعُ مَنْ يَكْـفرُك
Allaahumma Iyyaaka Na'budu, wa Laka nuswwaliy wa nasjudu, wa Ilayka nas'aa wa nahfidu, narjuu Rahmataka wa nakhshaa 'Adhaabak, Inna 'Adhaabaka bil-kaafiriyna mulhaqq. Allaahumma innaa Nasta'iynuka wa Nastaghfiruka, wa nuthniy 'Alaykal-khayra, wa laa Nakfuruka, wa nuuminu Bika, wa nakhdhwa'u Laka, wa Nakhla'u man Yakfuruka.
“Ee Allaah! Wewe tu ndiye tunayekuabudu, na Kwako tunaswali na tunasujudu, na Kwako tunakimbilia na tunakutumikia, tunataraji rehma Yako na tunaogopa adhabu Yako, kwani adhabu Yako hakuna shaka kuwa makafiri itawafikia. Ee Allaah! Hakika sisi tunakutaka msaada na tunakutaka msamaha na tunakusifu kwa kheri na wala hatukukufurishi na tunakuamini Wewe, na tunakunyenyekea na tunamuepuka anayekukufuru”

Na Allaah Anajua zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...