Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Hukumu ya Wudhuu kwa mwaamke aliyepaka kucha rangi

Swali: 

Ni ipi hukumu ya wudhuu´ kwa yule ambaye kwenye kucha zake amepaka rangi ya kucha?



Jibu: 


Rangi ya kucha ni kitu anachopaka mwanamke juu ya kucha na ni kitu kilicho na ukoko. 


Kwahiyo haijuzu kwa mwanamke kuitumia kipindi ambapo anaswali kwa kuwa inazuia maji kufika kwenye ngozi wakati wa kutawadha. 


Kila kitu kinachozuia maji kufika kwenye ngozi haijuzu kwa mwenye kutawadha kukitumia. Kwa kuwa Allaah amesema:
فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ
“Hivyo basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi.” (05:06)
Mwanamke huyu ambaye amepaka juu ya kucha zake rangi ya kucha yanazuia maji kufika kwenye ngozi. 


Kwa hivyo hawezi kusadikishwa ya kwamba ameosha mikono. Katika hali hiyo anakuwa ameacha kiungo cha faradhi wakati wa kutawadha au wakati wa kuoga.
Kuhusu wale wasioswali, kama mfano wa mwanamke mwenye hedhi, hakuna neno kuitumia. Isipokuwa ikiwa kama rangi hii ni katika mambo maalum ya makafiri. Katika hali hiyo itakuwa haijuzu kwa kuwa itakuwa ni kujifananisha.
Nimewasikia baadhi ya watu waliotoa fatwa ya kwamba rangi hii inaingia katika aina ya kuvaa soksi na kwamba inajuzu kwa mwanamke kuitumia kwa muda wa mchana mmoja na usiku wake kwa yule ambaye ni mkazi na kwa muda wa michana mitatu na nyusiku zake kwa yule amabaye ni msafiri. Fatwa hii ni ya kimakosa. 


Sio kila kitu kinachofunika miili ya watu kinaingizwa katika soksi. Shari´ah imekuja kufahamisha kuwa mtu anatakiwa kufuta juu ya khofu pindi mtu anapohitajia kufanya hivo. Mguu unahitajia kufunikwa na kusitiriwa kwa kuwa unagusa chini katika ardhi kwenye changarawe, baridi na mengineyo. 


Ndipo Shari´ah ikaja kusunisha kufuta juu yake. Mtu anaweza kutumia kipimo juu ya kilemba vilevile. Si sahihi kwamba kilemba mahala pake ni kichwani. 


Kimsingi ni kwamba ufutaji wa kwenye kichwa ni mwepesi. Ufaradhi wa kwenye kichwa ni kufuta tofauti na mkono ambao unatakiwa kuoshwa. 


Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumpa ruhusa mwanamke kufuta vifuniko vyake vya mikono (gloves) pamoja na kuwa vinafunika mikono. Hii ni dalili inayofahamisha kuwa haijuzu kwa mtu kutumia kipimo kwa kila kizuizi kinachozuia maji kufika na kikalinganishwa na kilemba na soksi.
Ni wajibu kwa muislamu kutumia juhudi zake katika kuitambua haki na wala asitoe fatwa yoyote isipokuwa atambue kuwa Allaah atamuuliza juu yake. Kwa kuwa mtu anaelezea kuhusu Shari´ah ya Allaah (´Azza wa Jall).


Marejeo : Majmuu´-ul-Fataawaa (11/147-148)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...