Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Sadaqah inafaa kumtolea mama yangu aliyefariki?

*Swali*

Jirani yangu aliniuliza kuhusu mama yangu aliye fariki kama nimemtolea sadaka baada ya kufa mimi nikamjibu sikutoa sadaka yoyote, isipokua mimi nijuavyo kama ana deni inabidi nimlipie ikiwa deni hilo ni kwa binaadamu au kwa Mwenyezi Mungu na kama aliweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga inabidi pia nimlipie kwa kufunga. Na zaidi na muombea dua yeye akanijibu haifai mtu akifiwa na mama yake inabidi amtolee sadaka ampelekee majuzuu na misahafu madrasa au msikitini sasa sijui uthibitisho wa hili.

*Jibu*

✅Maiti ananufaika kwa yote yaliyopitishwa na sheria ya Kiislamu ima katika Kitabu cha Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) na kwa uongofu wa Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

➡Imepokewa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Anapokufa mwanaadamu basi amali zake zote hukatika isipokuwa kwa mambo matatu: Sadaka ya kuendelea, au elimu yenye manufaa au mtoto mwema anayemuombea”
↪Imepokelewa na Imaam Muslim.

➡Ukitazama kwa hakika mambo yote hayo ni katika juhudi alizofanya maiti kabla ya kufa kwake. Hivyo, ujira wake unamwendea akiwa kaburini mwake.

✅Pia maiti ananufaika kwa yafuatayo kama alivyotuashiria Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Hakika kwa yanayomfuata Muumini kwa matendo na mambo mema baada ya mauti yake: Elimu aliyofundisha na kuieneza, mtoto mwema aliyemuacha, msahafu aliourithisha au Msikiti aliojenga, au nyumba kwa wapita njia aliyojenga, au sadaka aliyoitoa kutoka katika mali yake katika hali yake ya afya na uhai wake. Zote hizo zinamfuata baada ya umauti wake”
↪Imepokelewa na Imaam Ibn Maajah na Ibn Khuzaymah, na Isnadi yake ni Hasan.

✅Hizi Hadiyth mbili zinatuonyesha mambo yanayomnufaisha Muislamu anapokufa kwa mambo aliyoyafanya akiwa hai.

➡Lakini zipo Hadiyth zinazotueleza kuwa mtoto anapomtolea mzazi wake aliyefariki sadaka basi thawabu zinamfikia.

➡Miongoni mwazo ni: Yupo mtu aliyemuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Hakika mamangu ameaga dunia, je itamfaa nikimtolea sadaka?” Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ndio”.
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy.

➡Imepokewa kuwa Sa‘ad bin ‘Ubaadah (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema: “Ewe Mtume wa Allaah! Hakika mamake Sa‘ad amekufa, je ni sadaka ipi iliyo bora?” Akasema: “Maji”. Hivyo akachimba kisima akasema: “Cha mamake Sa‘ad”
↪Imepokelewa na Imaam Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah.

➡Na katika Hadiyth nyingine, alikuja mtu kwa Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: “Baba yangu amefariki na ameacha mali ambayo hakuusia chochote, je, nikitoa sadaka mali hiyo atapata malipo kwayo?” Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu: “Ndio”
↪Imepokelewa na Imaam Muslim

✅Hivyo yako mambo mengi ambayo yanamfaa maiti mojawapo ikiwa ni kumtolea sadaka na pia kumuombea duaa.

Na Allaah anajua zaidi

Imeandaliwa na *Imaam Masjid Tawbah*

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...