Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Fadhila za Kumswalia Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi Sallaam)

*Fadhila za Kumswalia Mtume Muhammad (Swallaah Allahu Aleyhi wa Sallaam)*

➡Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema⤵

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Nabiy. Enyi walioamini mswalieni na msalimieni kwa maamkizi ya amani na kwa tasliymaa. 
↪Surat Al-Ahzaab Aya ya 56.

✅Maana ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): *Ni kumsifia kwa Malaika, kumteremshia rahmah na baraka, fadhila nakadhalika.*

✅Maana ya Malaika Wake kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kumuombea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  *du’aa Amghufurie na Amteremshie baraka.* 

✅Maana ya Waumini kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni *kumuombea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) du’aa na amani.*

➡Juu ya hivyo Waumini kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inawarudia wenyewe thawabu tele kutokana na fadhila zilizotajwa katika Hadiyth kadhaa za Mtume Muhammad  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), miongoni mwazo ni⤵

عنْ عبد اللَّه بن عمرو بن العاص رضي اللَّه عنْهُمَا أنَّهُ سمِع رسُول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقُولُ: ((مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاَةً، صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عشْراً))  رواهُ مسلم

Imetoka kwa 'Abdullaah bin 'Amru bin Al'-Aasw (رضي الله عنهما)  kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Atakayeniswalia mara moja, Allaah Atamswalia mara kumi))
↪Imepokelewa na Imaam Muslim

*Al-Hadithi*

عن ابن مسْعُودٍ رضي اللَّه عنْهُ أنَّ رسُول اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال: ((أَوْلى النَّاسِ بي يوْمَ الْقِيامةِ أَكْثَرُهُم عَليَّ صلاةً)) رواه الترمذي وقال: حديثٌ حسنٌ

Imetoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Watu wa mwanzo kwangu (watakaokuwa karibu yangu) siku ya Qiyaamah ni wale wanaoniswalia sana)) 
↪Imepokelewa na Imaam At-Tirmidhy na kasema ni Hadiyth Hasan

*Al-Hadithi*

عنْ أبي هُريْرةَ رضي اللَّه عنهُ أنَّ رسُولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال: ((ما مِنْ أحد يُسلِّمُ علَيَّ إلاَّ ردَّ اللَّه علَيَّ رُوحي حَتَّى أرُدَّ عَليهِ السَّلامَ)) رواهُ أبو داود بإسناد صحيحٍ

Imetoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hapana yeyote atakayeniswalia ila Allaah Hurudishia mimi roho yangu hadi nimrudishie salaam (huyo aliyenisalimia)))
↪Imepokelewa na Imaam Abuu Daawuwd kwa Isnaad Hasan

✅Ndugu zangu katika Imaani, Tumuombe Allaah atujaalie tuwe ni wenye kuzipata fadhila hizi kwa Kumswalia kwa wingi Mtume wetu Muhammad (Swallaah Allahu Aleyhi wa Sallaam).

Na Allaah anajua zaidi

Imeandaliwa na *Imaam Masjid Tawbah*

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...