Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kujifuta Maji baada ya Kuoga na Kuchukua Wudhuu, Inajuzu?

Swali


Je nikishaoga bila kujikausha maji, nikatawadha halafu ndio nikajifuta mwili kwa taulosafi, itakuwa nimetengua udhu wangu? Au ni lazima nioge, nijikaushe kwanza kabla ya kutawadha?


Jibu 


Hakika kila ‘Ibaadah katika Uislamu ina utaratibu na nidhamu yake. Na wudhuu pia una utaratibu wake na vitu ambavyo vinatengua wudhuu huo. Ikiwa hakuna kitu chochote cha kutengua wudhuu basi jambo hilolitakuwa ni sawa.

Tukija moja kwa moja katika swali lako ni kuwa unaweza kuoga, kisha ukatawadha na mwisho ukafuta maji na wudhuu wako utakuwa ni sahihi kabisa.

Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake Al-Mughniy, anasema:
“Hakuna tatizo kukausha viungo kwa kutumia taulo baada ya kuoga au baada ya Wudhuu” Haya ndio yaliyopokelewa kutoka kwa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah). Imepokewa pia kuwa ‘Uthmaan bin ‘Affaan, Hasan bin ‘Aliy, ‘Aliy bin Abi Twaalib, Anas na Maswahaba wengine kuwa walikuwa wakitumia taulo kujikausha baada ya wudhuu.”

Shaykh Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) anasema kuwa,

“Hakuna makatazo yoyote ya mtu kujikausha baada ya wudhuu. Na endapo mtu atahoji vipi kuhusu Hadiyth ya mke wa Mtume, Maymuunah (Radhiya Allaahu ‘anha) kuwa alimletea Mtume taulo ajikaushe baada ya wudhuu na Mtume akakataa na akayapangusa maji mwilini mwake kwa mkono wake, basi jibu ni kuwa Hadiyth hiyo ina tafsiri nyingi na si kukataa kwa Mtume ni sababu kuwa haifai, bali sababu zinaweza kuwa nyingi kama vile, taulo kuwa chafu, au hakutaka kulilowesha taulo kwa maji ya mwilini mwake, au sababu zingine mbalimbali. Na kule Mke wake kumpa taulo kunaonyesha pia ni kuwa ni ada yake kuletewa taulo kujikausha nayo na kama si hivyo Mke wake asingempelekea hiyo taulokama jambo lenyewe halifai.” Majmu’ Fatawaa Ibn ‘Uthaymiyn (11/93)


Na Allaah Anajua zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Hukumu ya Wudhuu kwa mwaamke aliyepaka kucha rangi

Swali:  Ni ipi hukumu ya wudhuu´ kwa yule ambaye kwenye kucha zake amepaka rangi ya kucha? Jibu:  Rangi ya kucha ni kitu anachopaka mwanamke juu ya kucha na ni kitu kilicho na ukoko.  Kwahiyo haijuzu kwa mwanamke kuitumia kipindi ambapo anaswali kwa kuwa inazuia maji kufika kwenye ngozi wakati wa kutawadha.  Kila kitu kinachozuia maji kufika kwenye ngozi haijuzu kwa mwenye kutawadha kukitumia. Kwa kuwa Allaah amesema: فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ “Hivyo basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi.” (05:06) Mwanamke huyu ambaye amepaka juu ya kucha zake rangi ya kucha yanazuia maji kufika kwenye ngozi.  Kwa hivyo hawezi kusadikishwa ya kwamba ameosha mikono. Katika hali hiyo anakuwa ameacha kiungo cha faradhi wakati wa kutawadha au wakati wa kuoga. Kuhusu wale wasioswali, kama mfano wa mwanamke mwenye hedhi, hakuna neno kuitumia. Isipokuwa ikiwa kama rangi hii ni katika mambo maalum ya makafir...