Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tahiyyatul-Masjid inaweza kuswaliwa katika Nyakati zilizokatazwa?

Swali

Kuna mazungumzo mengi kuhusiana na Tahiyyatul Masjid. Kuna wanaosema haipaswi kutekelezwa nyakati zilizokatazwa kuswaliwa Swalaah, kama zile nyakati za kuchomoza jua, na kuzama jua.

Wengine husema inaruhusiwa maadam sababu ya kuswaliwa Swalaah hiyo, haijawekewa vikwazo vya nyakati zozote, na inapaswa kuswaliwa hata kama nusu ya jua litakuwa limeshazama.

Naomba ufafanuzi wa kina kwa suala hili.


Jibu

Naam kuna Ikhtilaaf  baina ya Wanachuoni kuhusu jambo hili.

Lakini mtazamo sahihi (Kauli yenye nguvu) ni kuwa, Tahiyyatul-Masjid ni rukhsa kuswaliwa katika nyakati zote, hata kama ni baada ya Al-Fajr au hata baada ya Al-‘Aswr kutegemea maana ya maneno ya jumla ya Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)⤵

“Atakapoingia yeyote katika nyinyi Msikitini, hapaswi kukaa hadi aswali rakaa mbili.”
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim

Vilevile, hiyo ni Swalaah ambayo ina sababu ya kuitekeleza kama vile Swalaah ya kutufu ‘Swalaatut-Twawaaf’ (Rakaa mbili zinazoswaliwa kufuatia kuzunguka Al-Ka’bah katika kipindi cha Hajj na ‘Umrah), na ‘Swalaatul-Kusuwf’ (Swalaah ya kupatwa kwa jua au mwezi), na rai iliyo sahihi ni kuwa, Swalaah zote hizi huweza kuswaliwa nyakati zozote zile zinapohitajika kuswaliwa hata kama ni katika zile nyakati ambazo zimekatazwa kuswaliwa Swalaah, kama vile ambavyo huswaliwa zile Swalaah za Fardhi za kulipwa ambazo mtu amezikosa, kwa mujibu wa maneno ya Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na Swalaah ya Twawaaf⤵

“Enyi watu (wa kabila la) ‘Abdi Manaaf! Msimzuie yeyote kufanya Twawaaf katika Nyumba hii, na kuswali nyakati zozote zile za usiku au mchana anapotaka.”
Imepokelewa na Imaam Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ahmad

➡Na amesema Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na Swalaah ya kupatwa kwa jua au mwezi⤵

“Hakika jua na mwezi ni alama mbili miongoni mwa alama za Allaah, hazipatwi kwa kifo au kuzaliwa mtu yeyote, hivyo, pindi unapoona hizo (zikipatwa), swali na uombe du’aa, hadi linapokusibu liondoke.”
Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim

➡Na kadhaalika, amesema Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)⤵

“Yeyote anayelala akapitwa na Swalaah au akasahau, basi alipe pindi tu atakapokumbuka, na hakuna kafara isipokuwa hiyo.” 
Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim

Hadiythi zote hizi, zinaonesha kujumuishwa nyakati ambazo Swalaah zimekatazwa kuswaliwa na nyakati nyinginezo.

Maelezo haya, yamefadhilishwa na Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah na mwanafunzi, Mwanachuoni mkubwa, Ibn Al-Qayyim (Rahimahumu Allaah).

Na Allaah ni mwenye kutoa Tawfiyq.

Rejea Kitab cha Imaam ‘Abdul-‘Aziyz Ibn Baaz, Fataawa Al-Islaamiyyah, juzuu ya 2, ukurasa namba 286

Imeandaliwa na Imaam Masjid Tawbah

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...