Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wudhuu unavunjika ikiwa Mtu hakujifunika Vizuri?

Swali

Je unapotia udhu ukiwa umevaa Bukta au suruali kipande imekufika mapajani tu. Udhu unaingia

Na vile vile kama   uko tumbo wazi kitovu kinaonekana una hio suruali kipande tu. Udhu Unafaa?


Jibu


Kutokujifunika vizuri sio miongoni mwa vitu vinavyovunja wudhuu. Yafutayo ni mambo yanayovunja wudhuu na yasiyovunja.

Yanayovunja wudhuu:  

1-Kutokwa na mkojo, kinyesi  au hewa katika sehemu za siri kutokana na dalili katika Qur-aan:
 ((أَوْ جَاء أَحَدٌ مَّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ))
((au mmoja wenu ametoka chooni)) [Al-Maaidah:6]
Vile vile Hadiyth:
         ((لا يقبل الله صلاة أحدكم إذا أحدث حتى يتوضأ )) البخاري   وسنن أبي داود  
((Allah Haikubali Swalah ya mmoja wenu akitokwa na haja hadi atawadhe)) [Al-Bukhaariy na Sunan Abu Daawuud]

2-Kutokwa na manii, madhii na wadii kutokana na dalili

 ما رواه علي بن أبي طالب رضي الله عنه قال : كنت رجلا مذّاء فأمرت المقداد أن يسأل  رسول الله صلى الله عليه وسلم فسأله فقال : ((فيه الوضوء ")) متفق عليه  
Kutoka  kwa  'Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu 'anhu)   ambaye amesema: "Nilikuwa ni mtu niliyekuwa nikitokwa sana na maji ya urethra (madhii). Nikamuambia Miqdaad amuulize Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)    kuhusu hilo. Akamuuliza na akasema : ((Inahiitajika kufanya wudhuu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

3-Usingizi mnono.

كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَأْمُرُنَا إِذَا كُنَّا سَفَرًا أَنْ لا نَنْزِعَ خِفَافَنَا ثَلاثَةَ أَيَّامٍ وَلَيَالِيهِنَّ إِلا مِنْ جَنَابَةٍ وَلَكِنْ مِنْ غَائِطٍ وَبَوْلٍ وَنَوْمٍ  -  
 رواه الترمذي   وحسنه الألباني -  فذكر النوم من نواقض الوضوء .
Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akituamrisha tunapokuwa safarini, tusivuwe khufu (viatu vya ngozi) zetu kwa muda wa masiku matatu, isipokuwa katika hali ya janaabah, lakini sio katika hali ya kuwa na kinyesi au mkojo au kulala)) [At-Tirmidhiy na amesema Shaykh Al-Abaaniy ni Hadiyth hasan].

Kwa hiyo Hadiyth hiyo inaonyesha kwamba usingizi ni mojawapo ya yanayovunja wudhuu.

4-Kupotewa na akili kwa sababu yoyote.

5-Kugusa sehemu za siri bila ya kukamatia kitu kwa  dalili ya Hadiyth ifuatayo:
           
بسرة بنت صفوان أنها سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم  يقول : (( من مسّ ذكره فليتوضأ ))
 رواه أبو داود  قال الألباني في صحيح سنن أبي داود صحيح   
Busra bin Swafwaan kwamba amemsikia Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Atakayeshika utupu wake atawadhe)) [Abu Daawuud na amesema Shaykh Al-Albaaniy katika Sahiyh Sunan Abu Daawuud, Sahiyh]  


Yasiyovunja wudhuu

1-Kumgusa mwanamke kwa ngozi
   
2- Kumwagikwa damu sehemu yoyote ya mwili isipokuwa damu ya hedhi au nifaas. Lakini kama kidonda, damu kutoka puani na kadhalika haivunji wudhu.

3-Kutapika ikiwa ni matapishi mengi au kidogo.

4-Unapokuwa na shaka ya kutokwa na kitu kamamkojo au hewa kutoka sehemu za siri baada ya kufanya wudhuu. Shaka hiyo ikiwa ni katika Swalah au nje ya Swalah. Lakini ukiwa una hakika kuwa umetokwa na kitu basi wudhuu utakuwa umevunjika.
ولذلك بوب البخاري رحمه الله بباب " لا يتوضأ من الشك حتى يستيقن " وجاء فيه حديث
عَبَّادِ بْنِ تَمِيمٍ عَنْ عَمِّهِ أَنَّهُ شَكَا إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الرَّجُلُ الَّذِي يُخَيَّلُ إِلَيْهِ أَنَّهُ يَجِدُ الشَّيْءَ
فِي الصَّلَاةِ  فَقَالَ : (( لا يَنْفَتِلْ أَوْ لا يَنْصَرِفْ حَتَّى يَسْمَعَ صَوْتًا أَوْ يَجِدَ رِيحًا ))"  الوضوء/134) ،
 فكل هذه الوساوس والتخيُّلات لا تنقض الوضوء
Al-Bukhaariy (Rahimahu Allah) ametenga mlango katika kitabu chake kauita 'Mtu asifanye wudhuu kwa ajili ya shaka hadi awe na uhakika'. Ametoa humo Hadiyth ya 'Abbaad bin Tamiym kutoka kwa ami yake kwamba, mtu alilalamika kwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba alidhania kwamba amehisi kitu kimemtoka wakati wa kuswali. Akasema: ((Usiache kuswali) ila kamaumesikia sauti au harufu))
       
Kwahiyo  Wasi wasi na dhanakama hizi hazivunji wudhuu. 

    5-Kucheka kwa nguvu akiwa katika Swalah haivunjui wudhuu bali inavunja  Swalah.

6-Kuosha maiti hakuhitaji kufanya wudhuu ila inapendekezeka tu pamoja na kukoga josho (ghuslu)

Na Allaah Anajua Zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Hukumu ya Wudhuu kwa mwaamke aliyepaka kucha rangi

Swali:  Ni ipi hukumu ya wudhuu´ kwa yule ambaye kwenye kucha zake amepaka rangi ya kucha? Jibu:  Rangi ya kucha ni kitu anachopaka mwanamke juu ya kucha na ni kitu kilicho na ukoko.  Kwahiyo haijuzu kwa mwanamke kuitumia kipindi ambapo anaswali kwa kuwa inazuia maji kufika kwenye ngozi wakati wa kutawadha.  Kila kitu kinachozuia maji kufika kwenye ngozi haijuzu kwa mwenye kutawadha kukitumia. Kwa kuwa Allaah amesema: فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ “Hivyo basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi.” (05:06) Mwanamke huyu ambaye amepaka juu ya kucha zake rangi ya kucha yanazuia maji kufika kwenye ngozi.  Kwa hivyo hawezi kusadikishwa ya kwamba ameosha mikono. Katika hali hiyo anakuwa ameacha kiungo cha faradhi wakati wa kutawadha au wakati wa kuoga. Kuhusu wale wasioswali, kama mfano wa mwanamke mwenye hedhi, hakuna neno kuitumia. Isipokuwa ikiwa kama rangi hii ni katika mambo maalum ya makafir...