Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Damu ya ugonjwa ilioambatana na hedhi

        Damu ya ugonjwa ilioambatana na hedhi




Damu ya ugonjwa ina hali tatu ambazo ni:

Hali ya kwanza Mwanamke ana hedhi yenye kujulikana kabla ya damu ya ugonjwa. Katika hali hii atatendea kazi hedhi yake na hukumu zake. Ile damu yenye kuzidi ni damu ya ugonjwa ambayo itatendewa kazi kutokana na hukumu zake.
Mfano wa hilo mwanamke anapata hedhi zile siku sita za mwanzo wa kila mwezi. Kisha baada ya hapo akapata damu ya ugonjwa yenye kuendelea. Katika hali hii hedhi yake ni zile siku sita za mwanzo wa kila mwezi na ile nyingine yote ni damu ya ugonjwa. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
“Faatwimah bint Abiy Hubaysh alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia: “Ee Mtume wa Allaah! Mimi ni mwanamke nisiyetwaharika. Je, niache kuswali?” Akasema: “Hapana. Huo ni mshipa na wala si hedhi. Pale hedhi yako inapokuja basi acha swalah. Wakati inapomalizika jitwaharishe kisha swali.”Al-Bukhaariy (306).


Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” yake kuwa Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Himnah bint Jahsh:
“Kaa kiasi cha hedhi inavyokuzuia. Kisha baada ya hapo oga na uswali.”Muslim (334).

Kutokana na hili mwanamke ambaye yuko na damu ya ugonjwa na ana hedhi yenye kujulikana atakaa kiasi cha hedhi inavyomzuia. Baada ya hapo ataoga na kuswali na kupuuza damu inayotoka.



Hali ya Pili Mwaname kutokuwa na hedhi yenye kujulikana kabla ya kupata damu ya ugonjwa kwa njia ya kwamba damu yake ya ugonjwa inaendelea kuanzia pale anapopata damu yake ya kwanza. 


Mwanamke huyu anatakiwa kupambanua kati ya ile damu ya kwanza na ya pili. Hedhi yake ni ile nyeusi, nzito na yenye kunuka. Katika hali hii hapa kunatumika hukumu za hedhi. Ile nyingine yote ni damu ya ugonjwa ambayo ina hukumu zake.

Mfano wa hilo mwanamke anapata damu kwa mara ya kwanza na haikatiki. Hata hivyo damu yake zile siku kumi za mwanzo ni nyeusi na siku zilizosalia za mwezi ni nyekundu, nzito zile siku kumi za mwanzo na khafifu siku zilizosalia za mwezi au ni yenye kunuka zile siku kumi za mwanzo na siku zilizosalia za mwezi sio yenye kutoa harufu. 


Katika hali hii ana hedhi pale ambapo damu ni nyeusi katika mfano wa kwanza, nzito katika mfano wa pili na yenye kunuka katika mfano wa tatu. Nyingine yote ni damu ya ugonjwa. 


Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Faatwimah bint Abiy Hubaysh:
“Ikiwa ni damu ya hedhi, ni nyeusi na inajulikana. Ikiwa ni hivyo basi usiswali. Na ikiwa ni nyingine tawadha na uswali. Huo ni mshipa tu.”Abu Daawuud (286), an-Nasaa´iy (216) na (363) na al-Haakim (1/174). Ibn Haajar amesema katika ”at-Talkhiys: ”Iko kwa masharti ya Muslim.”



Hali ya Tatu Mwanamke kutokuwa na hedhi yenye kujulikana na upambanuzi uliosalama. Kwa maana ya kwamba damu yake ya ugonjwa inakuwa ni yenye kuendelea tangu pale anapopata damu yake ya kwanza kwa sifa moja au kwa sifa zenye kutofautiana kwa kiasi cha kwamba haiwezi kuwa hedhi. Hapa atafanya kama wanavofanya wanawake wengi. 


Bi maana atafanya hedhi yake ni siku sita au saba kwa mwezi. Inaanza pale anapoanza kupata damu. Nyingine yote ni damu ya ugonjwa.

Mfano wa hilo apate damu siku ya tano katika mwezi. Damu hiyo iendelee kutiririka na wakati huo huo hawezi kuona upambanuzi wa wazi wenye kuashiria kuwa ni damu ya hedhi. Hakuna chenye kusaidia si rangi wala sifa nyingine. Katika hali hii hedhi yake itakuwa siku sita au saba na inaanza tangu siku ya tano katika kila mwezi. Dalili ya hilo ni Hadiyth ya Himnah bint Jahsh (Radhiya Allaahu ´anhaa):
“Ee Mtume wa Allaah! Mimi nina damu ya ugonjwa kubwa na yenye nguvu. Unasemaje juu yake? Imenizuia kuswali na kufunga.” Mtume akasema: “Chukua pamba na weka kwenye tupu. Inaondosha damu.” Akasema: “Ni zaidi ya hivyo.”
Katika Hadiyth hiyo hiyo Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:
Hakika haya ni masumbufu ya shaytwaan. Una hedhi siku sita au saba kwa mujibu wa ujuzi wa Allaah (Ta´ala). Kisha oga. Pale utakapoona umetwaharika kabisa swali siku ishirini na nne au ishirini na tatu na ufunge siku ishirini na nne au ishirini na tatu.”Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy ambaye amesema kuwa ni Swahiyh. Imenukuliwa kutoka kwa Ahmad kwamba amesema kuwa ni Swahiyh wakati al-Bukhaariy amesema kuwa ni nzuri.


Maneno ya Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) “siku sita au saba” hamaanishi kufanya khiyari bali vile atavyoonelea kuwa ndio karibu na usawa. Ataidurusu hali yake na kuchagua lile analoona kuwa ni lenye kuafikiana bora zaidi na wanawake wenye kufanana naye kwa njia ya kimaumbile, miaka na chimbuko, kile ambacho katika damu yake kimekaribia damu ya hedhi na mambo mengine yenye uwezekano. Akiona kuwa kilicho karibu ni siku sita, afanye kuwa siku sita, na akiona kilicho karibu ni siku saba, afanye kuwa ni siku saba.


Rejea Kitaab  Ad-Dimaa' at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa' 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Mume kunyonya maziwa ya mkewe inafaa...?

Swali Mume kunyonya maziwa (matiti) ya mkewe inafaa...? Jibu Hakuna Uharamu wa Mume  kunyonya matiti ya mke wake.  Allaah(Subhaana wa Taala) Anasema kwamba:  ((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ وَاعْلَمُواْ أَنَّكُم مُّلاَقُوهُ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ)) ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Allaah , na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wape bishara njema Waumini)) [2:223] Kwahiyo mwanamke anayo ruhusa ya kumchezea mkewe sehemu yoyote ya mwili wake pamoja na kunyonya maziwa ya mkewe isipokuwa tu Kufanya naye jimai kwa sehemu ya nyuma (liwati). Aayah hii:  “ Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. “   imeteremka kuhusu Mayahudi waliokuwa wakisema kuwa mwanaume akimuingilia mke wake kupitia upande wa nyuma basi anazaliwa mtoto akiwa ana makengeza. Ndipo i

Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye Muziki na Vinanda

Swali Inafaa Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye  Muziki na Vinanda Jibu  Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu hukumu ya muziki inayotiwa katika Nashiyd na Qaswiydah. Muziki na utumiaji wa ala za muziki ni haramu katika Dini yetu hii, Uislamu. Zifuatazo ni dalili kuhusu hilo:   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Kutakuwa watu katika Ummah wangu watakao halalisha uzinzi, uvaaji wa Hariri, pombe (unywaji) na ma’aazif (ala za muziki) ” (al-Bukhaariy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Mwisho wa zama (dunia) kutakuwa na maporomoko ya ardhi, mawe kutoka mbinguni na kugeuza kwa wanyama, wakati ambapo ala za muziki na waimbaji wanawake watakapoenea na pombe kuruhusiwa ” (atw-Twabaraniy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Watu katika ummah wangu watakunywa pombe, kuiita kwa jina jingine. Watatiwa furaha kwa uchezaji wa ala za muziki na uimbaji wa wanawake (watakao

Hukumu ya Mke kutoka nyumbani bila Ruksa ya mumewe

Naam shukrani kwa swali lako kuhusu mkeo kutoka bila ya ruhusa yako kwenda katika mishuari zake. Matatizo haya hutokea mara nyingi kwa mke kutokuwa na ufahamu na ujuzi wa Dini ya Kiislamu. Au mara nyingine huwa kweli ana elimu lakini hushindwa kufuata kimatendo kwa sababu moja au nyingine. Au huenda akawa na elimu, lakini akakosa Dini. Kwa ajili hiyo Imaam al-Bukhaariy, ana mlango katika  Swahiyh  yake wenye kichwa cha habari, “ Elimu Kabla Ya ‘Amali ”. Hata hivyo, huenda mtu akawa na elimu lakini akawa hana ‘amali kwa sababu ya kutokuwa na ikhlaasw.   Ni juu ya mke kumtii mumewe katika mambo yasiyo ya maasi, kwani hakuna utiifu katika maasiya. Ikiwa mume hakutoa ruhusa mbali na kuwa yu mbali na mkewe ni wajibu wa mke kutii amri hiyo. Hata hivyo, haifai kwa mume kuweka vikwazo vya kupita kiasi,  kama kumzuia kwenda kwa wazazi wake na mahali ambapo anaweza kupata elimu ya Kidini. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “ Wakikutiini, basi msiwatafutie njia ” (an-Nisaa’ [4]: 34). Hii