Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Haijuzu kwa mke kubaki na mume kafiri asiyeswali

Swali


Tatizo langu ni kuhusiana na mume wangu, ni mwanaume ambaye ana mapungufu katika Dini yake, haswali. Na pindi ninapomwita kuswali anakasirika na ananifanyia istihzai. Na anaendelea kuacha Swalah kwa hoja kuwa baba yake alikuwa haswali, hii ndio sababu na yeye haswali. Niliendelea na hali ya kumkumbusha na siku moja akanambia: “Ukiendelea kwa hali hii, mlango uko wazi”, hapo ndio nilifika namuomba Talaka. Na mara ya pili ilikuwa takriban sababu hiyo hiyo. Akanambia: “Usiniongeleshi mpaka siku ya Qiyaamah”. Ipi rai yako kwa mtu huyu na kwa maneno yake aliyosema kwa minasaba miwili, wa kwanza na wa pili? Je, huchukuliwa ni Talaka au nini? Na je, inajuzu kwangu kubaki nae katika hali hii?


Jibu



Mwanaume huyu haijuzu kubaki nae. Maadamu anaacha Swalah kama ulivyosema, kwa hilo anakuwa kafiri. Ikiwa baba yake naye haswali, kaiga kwake. Na wala haijuzu kumuiga kafiri asiyeswali, anatukana Dini, au anafanya kitu miongoni mwa vitu vinavyovunja Uislamu wa mtu au maasi katika maasi ya kumuasi Allaah. Watu wote hawa ni mamoja. Mwanaume huyu ni kafiri na kamuiga kafiri mwenzake kutokana na kauli yake. Na imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba kasema:
“Baina ya mtu na baina ya kufuru na Shirki ni kuacha Swalah.” (Kaipokea Muslim katika Swahiyh yake)
Na kasema (´alayhis-Swalaah was-Salaam):
“Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni Swalah, mwenye kuiacha amekufuru.”

Kauli yenye nguvu katika kauli za wanachuoni ni kwamba, mwenye kuiacha kwa kuzembea na uvivu ni kafiri, hata kama hakupinga uwajibu wake. Na ikiwa mwanaume huyu anapinga uwajibu wake, ni kafiri kwa Ijmaa´. 


Kwa hali yoyote, mwanaume huyu ni mwanaume mbaya na ni kafiri kwa kuacha kwake Swalah kutokana na kauli yenye nguvu ya wanachuoni. Haijuzu kwako kubaki nae. Bali ni wajibu kwako kuachana nae na wala usimpe kitu. Na kauli yake kusema kuwa mlango uko wazi, hii ni kinaya. Ikiwa amekusudia Talaka, anakusudia utoke kwa nia ya Talaka, itakuwa ni Talaka. 


Na ikiwa hakukusudia Talaka, itakuwa sio Talaka. Lakini kwa hali yoyote, hata kama hakukutaliki, haitakikani kwako kubaki nae. 


Bali ni wajibu kwako kumuacha na umuachie [… sauti haiko wazi… ], na watoto wako uwachukue na yeye (mume) hana haki ya (kubaki na) watoto kutokana na ukafiri wake. Wewe ndiye aula zaidi ya watoto wako. 


Ni mwanaume mbaya kwa kumkufuru kwake Allaah (´Azza wa Jalla). Huenda Allaah Akamsamehe. Akitubu nawe bado ungali ndani ya eda, akarejea, akatubu kwa Allaah na akajuta kwa aliyoyafanya na akaanza kuswali, hakuna ubaya kwako kurudi kwake na maadamu ungali ndani ya eda. Ama baada ya eda hapana (kurudi kwake), isipokuwa kwa ndoa mpya.



Na  Allaah  anajua  zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...