Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Hukumu ya damu ya ugonjwa

                  Hukumu ya damu ya ugonjwa




Tumeshatangulia kujua ni vipi tutatofautisha damu ya hedhi na damu ya ugonjwa. Pindi damu ni hedhi inakuwa na hukumu za hedhi na pindi damu ni ya ugonjwa inakuwa na hukumu ya damu ya ugonjwa. Tumeshatangulia kutaja hukumu muhimu zenye kufungamana na damu ya hedhi.

Ama kuhusiana na hukumu ya damu ya ugonjwa, ni hukumu zile zile kama katika kipindi cha utwaharifu. Hakuna tofauti kati ya mwanamke aliye na damu ya ugonjwa na mwanamke mtwaharifu isipokuwa katika mambo yafuatayo:
Jambo la kwanza Ni wajibu kwake kutawadha katika kila swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kisha tawadha kwa kila swalah.”Al-Bukhaariy (228)


Ina maana ya kwamba asitawadhe kwa ajili ya kuswali swalah iliyowekewa nyakati maalum isipokuwa baada ya kuwa wakati wake umeshaingia. Hata hivyo ni sawa akatawadha pale anapotaka kuswali swalah ambayo haikuwekewa nyakati maalum.
Jambo la Pili Anapotaka kutawadha anatakiwa kuosha athari ya damu ukeni na kuweka pamba ili izuie damu. Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Chukua pamba na weka kwenye tupu. Inaondosha damu.” Akasema: “Ni zaidi ya hivyo.” Mtume akasema: “Chukua kitambaa.” Akasema: “Ni zaidi ya hivyo.” Mtume akasema: “Izuie basi.”Abu Daawuud (287), at-Tirmidhiy (128) na Ahmad (6/382).


Damu itayotoka baada ya hapo haidhuru kitu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Faatwimah bint Abiy Hubaysh:
“Usiswali unapokuwa na hedhi. Baada ya hapo koga na utawadhe kwa kila swalah na uswali hata kama damu itadondoka kwenye jamvi.”Ahmad (6/42) na Ibn Maajah (624).



Jambo la Tatu  Jimaa. Wanachuoni wana maoni mbali mbali kuhusu jimaa kama hakukhofiwi dhambi. Maoni ya sawa ni kuwa inajuzu kabisa. Sio chini ya wanawake kumi walikuwa na damu ya ugonjwa katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini si Allaah wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwakataza kufanya jimaa. Bali katika Kauli Yake Allaah (Ta´ala):
فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ
“… basi waepukeni wanawake [wanapokuwa] katika hedhi. Wala msiwakaribie [kujimai nao] mpaka watwaharike.” (02:222)
kuna dalili kuwa vinginevyo sio wajibu kuwaepuka. Ikiwa anapata kuswali basi vivyo hivyo anapata kufanya jimaa. Si sahihi kulinganisha jimaa yake na jimaa ya mwanamke mwenye hedhi kwa sababu hawako hata sawa kwa wale wenye kuonelea kuwa ni haramu. Ulinganisho hausihi ikiwa unakosa ufanano wa karibu.




Na Allaah  anajua  zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Mume kunyonya maziwa ya mkewe inafaa...?

Swali Mume kunyonya maziwa (matiti) ya mkewe inafaa...? Jibu Hakuna Uharamu wa Mume  kunyonya matiti ya mke wake.  Allaah(Subhaana wa Taala) Anasema kwamba:  ((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ وَاعْلَمُواْ أَنَّكُم مُّلاَقُوهُ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ)) ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Allaah , na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wape bishara njema Waumini)) [2:223] Kwahiyo mwanamke anayo ruhusa ya kumchezea mkewe sehemu yoyote ya mwili wake pamoja na kunyonya maziwa ya mkewe isipokuwa tu Kufanya naye jimai kwa sehemu ya nyuma (liwati). Aayah hii:  “ Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. “   imeteremka kuhusu Mayahudi waliokuwa wakisema kuwa mwanaume akimuingilia mke wake kupitia upande wa nyuma basi anazaliwa mtoto akiwa ana makengeza. Ndipo i

Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye Muziki na Vinanda

Swali Inafaa Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye  Muziki na Vinanda Jibu  Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu hukumu ya muziki inayotiwa katika Nashiyd na Qaswiydah. Muziki na utumiaji wa ala za muziki ni haramu katika Dini yetu hii, Uislamu. Zifuatazo ni dalili kuhusu hilo:   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Kutakuwa watu katika Ummah wangu watakao halalisha uzinzi, uvaaji wa Hariri, pombe (unywaji) na ma’aazif (ala za muziki) ” (al-Bukhaariy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Mwisho wa zama (dunia) kutakuwa na maporomoko ya ardhi, mawe kutoka mbinguni na kugeuza kwa wanyama, wakati ambapo ala za muziki na waimbaji wanawake watakapoenea na pombe kuruhusiwa ” (atw-Twabaraniy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Watu katika ummah wangu watakunywa pombe, kuiita kwa jina jingine. Watatiwa furaha kwa uchezaji wa ala za muziki na uimbaji wa wanawake (watakao

Hukumu ya Mke kutoka nyumbani bila Ruksa ya mumewe

Naam shukrani kwa swali lako kuhusu mkeo kutoka bila ya ruhusa yako kwenda katika mishuari zake. Matatizo haya hutokea mara nyingi kwa mke kutokuwa na ufahamu na ujuzi wa Dini ya Kiislamu. Au mara nyingine huwa kweli ana elimu lakini hushindwa kufuata kimatendo kwa sababu moja au nyingine. Au huenda akawa na elimu, lakini akakosa Dini. Kwa ajili hiyo Imaam al-Bukhaariy, ana mlango katika  Swahiyh  yake wenye kichwa cha habari, “ Elimu Kabla Ya ‘Amali ”. Hata hivyo, huenda mtu akawa na elimu lakini akawa hana ‘amali kwa sababu ya kutokuwa na ikhlaasw.   Ni juu ya mke kumtii mumewe katika mambo yasiyo ya maasi, kwani hakuna utiifu katika maasiya. Ikiwa mume hakutoa ruhusa mbali na kuwa yu mbali na mkewe ni wajibu wa mke kutii amri hiyo. Hata hivyo, haifai kwa mume kuweka vikwazo vya kupita kiasi,  kama kumzuia kwenda kwa wazazi wake na mahali ambapo anaweza kupata elimu ya Kidini. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “ Wakikutiini, basi msiwatafutie njia ” (an-Nisaa’ [4]: 34). Hii