Ruka hadi kwenye maudhui makuu

kuvumilia maudhi ya wanawake wanapokuwa wajawazito

Swali: Mimi nilioa na tahamaki mke wangu akaniomba talaka kwa hoja kwamba hakuishi maisha ya starehe vile alivyotarajia. Mimi ni kijana na mwanafunzi vilevile ambaye hali yangu ni ya kawaida. Kuniomba kwake talaka kulikuwa ni pasi na haki na mimi sikuwa na nia ya kumtaliki kwa kuwa alikuwa ni mjamzito. Je, akiniomba talaka ni haki kwangu kurudishiwa mahari? Isitoshe mahari yenyewe ilikuwa ni misaada kutoka kwa watu. Je, ikiwa atanipa mahari hayo nina haki ya kuzitumia au nitatakiwa kuzirudisha kule nilikozichukua pamoja na kuwa mimi ni mwenye madeni tele yasiyojua yeyote isipokuwa Allaah pekee.



Jibu: Katika hali hii mwanaume akiweza kuwa na subira na asimjibu ndio bora zaidi. Hili ni kwa sababu mbili:


Ya kwanza: Baadhi ya wanawake wanapokuwa na mimba wanawachukia waume zao. Wanawachukia waume zao hata kama ameishi naye miaka mingi. Kwa hivyo awe na subira juu yake mpaka yataisha. Huenda akarudi katika hali yake ya kawaida na yakamuondoka yaliyomkereta moyoni mwake.

Ya pili: Huenda baada ya kujifungua akaelewa kuwa anatakiwa kubaki kwa mume wake na hatimaye yakamwondoka yaliyomo moyoni mwake.
Mimi naona kwamba ikiwa amemridhia tabia na dini yake basi awe na subira juu yake na amfanyie wepesi mpaka migogoro iishe. Baada ya yeye kujifungua ataangaliwa kama kweli anaona hawezi kubaki basi ni sawa akaomba haki yake. Mwanamke wa Thaabit bin Qays (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia:
“Ee Mtume wa Allaah! Sina cha kumtia dosari Thaabit bin Qays si katika tabia wala dini. Lakini mimi nachelea kufuru katika Uislamu.”
Kumesemwa tabia na dini. Isitoshe huyu ni miongoni mwa wale ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemshuhudilia Pepo.
Aliposema kuwa anachelea kufuru katika Uislamu bi maana kwamba hawezi. Hapo ndipo alipomwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Je, utaweza kumrudishia bustani yake?” Akajibu: “Ndio.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwita na kumwambia: “Chukua bustani yako na umtaliki.”
Akachukua bustani yake na kumtaliki. Kwa hivyo tunamshauri mwanaume huyu asubiri mpaka pale mwanamke huyu atapojifungua. Huenda vilevile akabadilika baada tu ya kujifungua midhali ameridhika na dini na tabia yake. Vinginevyo mambo yasipobadilika basi hakuna ubaya kwake akamuomba haki yake yote aliyompa kuanzia mahari, zawadi na vinginevyo. 


Ikiwa baadaye atarudi kwake basi hivyo vitu ni vya mwanaume kwa kuwa alivichukua kwa haki. Ikiwa alivichukua kwa haki yake basi yeye ndiye mwenye kuvimiliki. Wakati mwanaume alipovichukua kwa ajili ya ndoa amekuwa ni mwenye kuvimiliki. Vikirudi kwake basi ni miliki yake. Katika hali hii sio wajibu kwake kuvirudisha kwa yule aliyevichukua kutoka kwake.



Rejea al-Liqaa' ash-Shahriy (31)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...