Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Talaka za Bid´ah

Swali


Tumejua kupitia barnamiji hii ya kwamba haipiti Talaka kwa mwenye hedhi na mwenye mimba. Je, ni kuwa haipiti kabisa au inapita baada ya Twahara?



Jibu



Talaka ya mwenye hedhi haipiti kutokana na kauli sahihi (yenye nguvu) ya wanachuoni, tofauti na kauli ya jamhuri. Jamhuri ya wanachuoni wanaona kuwa inapita. Hali kadhalika kwa mwenye nifasi. 


Lakini kauli ya sahihi katika kauli za wanachuoni, na ndio waliokuwa wakifutu baadhi ya Taabi´iyn na Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na akaichagua Shayk-ul-Islaam bin Taymiyyah, mwanafunzi wake Ibn al-Qayyim na kundi katika wanachuoni, kuwa Talaka hii haipiti. Kwa kuwa inakwenda kinyume na Shari´ah ya Allaah, kwa kuwa Allaah Kawekea Shari´ah kumtaliki mwanamke katika hali ya Twahara ya nifasi, hedhi na katika Twahara ambayo mume wake hakumjamii. 


Hii ndio Talaka ya Kishari´ah. Akimtaliki katika hedhi, nifasi au Twahara ambayo amemjamii, Talaka hii ni Bid´ah na wala haipiti kutokana na kauli ya sahihi ya wanachuoni. Kwa Kauli ya Allaah (Jalla wa ´Alaa):
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ
“Ee Nabii! Mtakapowataliki wanawake, basi watalikini katika wakati wa eda (twahara na si katika hedhi) zao.” (65:01)
Bi maana katika Twahara ya jimaa. Namna hii ndivyo walivyosema wanachuoni kuhusu (maana ya) “watalikini katika wakati wa eda.” Wawe Twahara hawakuingiliwa au wawe na ujauzito. 



Hii ndio Talaka ya katika eda. Ama Talaka ya mjamzito wanachuoni wanaona kuwa inapita, na mwenye kusema kuwa haipiti kakosea. Talaka ya mjamzito inapita kwa wanachuoni, Talaka isiyopita ni ya mwenye hedhi na nifasi na Twahara ambayo mwanamke kaingiliwa na hakujadhihiri mimba yake. 



Talaka hizi (sampuli tatu) hazipiti kutokana na kauli ya sahihi ya wanachuoni, kwa kuwa zinakhalifu na Shari´ah ya Allaah na vile vile ni katika hali ambayo haikuwekwa Talaka kama tulivyotangulia kusema. Na baadhi ya ´Awwaam wanastaajabu na kusema Talaka ya mjamzito haipiti, hili ni kosa. Hii ni katika kauli za ´Awwaam zisizokuwa na asli katika Shari´ah wala maneno ya wanachuoni. Mjamzito Talaka inapita. Ni wajibu kujua hilo.

Rejea Nuur ´alaad-Darb

Na  Allaah anajua  zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...