Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Hadiyth pekee iliyosihi kuhusu Kursiy

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mbingu saba ukizilinganisha na Kursiy si kitu isipokuwa ni kama mfano wa kijipete cha chuma kilichotupwa katika uwanja mkubwa. ´Arshi ukiilinganisha na Kursiy ni kama huo uwanja mkubwa ukiulinganisha na kijipete hicho.”
Ameipokea Muhammad bin Abiy Shaybah katika “Kitaab-ul-´Arsh”1/114.



Hadiyth kwa njia zote hizi ni Swahiyh.
Hadiyth ni dalili ya wazi yenye kuonyesha kwamba Kursiy ndio kiumbe kikubwa zaidi baada ya ´Arshi na kwamba ni kitu kilichosimama kivyake na si kitu cha kimaana. Hapa kuna Radd kwa wale wenye kufasiri Kursiy kwamba ni ufalme na utawala ulioenea, kama ilivyotajwa katika baadhi ya tafsiri ya Qur-aan. Imepokelewa kutoka kwa Ibn ´Abbaas alisema kuwa ni elimu, lakini cheni ya wapokezi wake si Swahiyh. Katika cheni ya wapokezi yupo Ja´far  bin Abiyl-Mughiyrah ambaye kapokea kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr ambaye kapokea kutoka kwa Ibn ´Abbaas. Upokezi huo umepokelewa na Ibn Jariyr. Ibn Mandah amesema:
“Ibn Abiyl-Mughiyrah si mwenye nguvu kabisa inapokuja kwa Ibn Jubayr.”Tazama ”adh-Dhwa´iyfah” (2/307).


Tambua kwamba hakukusihi kitu kuhusu Kursiy isipokuwa Hadiyth hii tu. Zipo Hadiyth zinazosema kwamba Kursiy ni mahali pa kuwekea miguu, kwamba ina sauti kama kitako cha farasi, kwamba inabebwa na Malaika wane ambapo kila Malaika ana nyuso nne na nyoyo zao ziko chini ya mwamba ulioko chini ya ardhi ya saba na kadhalika. Hakuna chochote katika hayo kilichosihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).


Rejea Kitaab Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (1/1/226)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Mume kunyonya maziwa ya mkewe inafaa...?

Swali Mume kunyonya maziwa (matiti) ya mkewe inafaa...? Jibu Hakuna Uharamu wa Mume  kunyonya matiti ya mke wake.  Allaah(Subhaana wa Taala) Anasema kwamba:  ((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ وَاعْلَمُواْ أَنَّكُم مُّلاَقُوهُ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ)) ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Allaah , na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wape bishara njema Waumini)) [2:223] Kwahiyo mwanamke anayo ruhusa ya kumchezea mkewe sehemu yoyote ya mwili wake pamoja na kunyonya maziwa ya mkewe isipokuwa tu Kufanya naye jimai kwa sehemu ya nyuma (liwati). Aayah hii:  “ Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. “   imeteremka kuhusu Mayahudi waliokuwa wakisema kuwa mwanaume akimuingilia mke wake kupitia upande wa nyuma basi anazaliwa mtoto akiwa ana makengeza. Ndipo i

Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye Muziki na Vinanda

Swali Inafaa Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye  Muziki na Vinanda Jibu  Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu hukumu ya muziki inayotiwa katika Nashiyd na Qaswiydah. Muziki na utumiaji wa ala za muziki ni haramu katika Dini yetu hii, Uislamu. Zifuatazo ni dalili kuhusu hilo:   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Kutakuwa watu katika Ummah wangu watakao halalisha uzinzi, uvaaji wa Hariri, pombe (unywaji) na ma’aazif (ala za muziki) ” (al-Bukhaariy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Mwisho wa zama (dunia) kutakuwa na maporomoko ya ardhi, mawe kutoka mbinguni na kugeuza kwa wanyama, wakati ambapo ala za muziki na waimbaji wanawake watakapoenea na pombe kuruhusiwa ” (atw-Twabaraniy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Watu katika ummah wangu watakunywa pombe, kuiita kwa jina jingine. Watatiwa furaha kwa uchezaji wa ala za muziki na uimbaji wa wanawake (watakao

Hukumu ya Mke kutoka nyumbani bila Ruksa ya mumewe

Naam shukrani kwa swali lako kuhusu mkeo kutoka bila ya ruhusa yako kwenda katika mishuari zake. Matatizo haya hutokea mara nyingi kwa mke kutokuwa na ufahamu na ujuzi wa Dini ya Kiislamu. Au mara nyingine huwa kweli ana elimu lakini hushindwa kufuata kimatendo kwa sababu moja au nyingine. Au huenda akawa na elimu, lakini akakosa Dini. Kwa ajili hiyo Imaam al-Bukhaariy, ana mlango katika  Swahiyh  yake wenye kichwa cha habari, “ Elimu Kabla Ya ‘Amali ”. Hata hivyo, huenda mtu akawa na elimu lakini akawa hana ‘amali kwa sababu ya kutokuwa na ikhlaasw.   Ni juu ya mke kumtii mumewe katika mambo yasiyo ya maasi, kwani hakuna utiifu katika maasiya. Ikiwa mume hakutoa ruhusa mbali na kuwa yu mbali na mkewe ni wajibu wa mke kutii amri hiyo. Hata hivyo, haifai kwa mume kuweka vikwazo vya kupita kiasi,  kama kumzuia kwenda kwa wazazi wake na mahali ambapo anaweza kupata elimu ya Kidini. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “ Wakikutiini, basi msiwatafutie njia ” (an-Nisaa’ [4]: 34). Hii