Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kwa nini Mtu akila Nyama ya Ngamia Wudhuu unatenguka?

SWALI LA KWANZA:

Bismillah rahmani rahim.
Namshukuru Allah Muumba wa ulimwengu kwa kunikubalia kujiunga na mtandao huu (Allhamdullillahi Rabill allamina)
 
Swali: Katika kusoma FisabililLaah Blog nimesoma kuwa "Ukila nyama ya Ngamia kama umetia "udhu" basi udhu unatenguka. Kwa nini
Nitafurahi sana ikiwa utanielezea na Hadith za maswahaba

Shukran. Allhamdullillahi Rabill allamina.


SWALI LA PILI:

Assalam Aalaykum: Allah Awabariki kwa jitihada zenu Amin.

Nina Swali kuhusu Ngamia. niliingia katika web hii nikatafuta katika sehemu ya kujifinza au namna ya kutia wudhuu. Nikaangalia Step baada ya Step. Mwisho Mukaweka Mambo yanayotengua Wudhuu. Na mukatoa mifano. Kama Kujamba. kwenda haja kubwa. Mkojo. Na kula Nyama ya ngamia. Sasa Naomba Hadith zinazoelezea kuhusu kutokwa na Wudhuu Unapokula Nyama ya Ngamia.
Niliingia vivile sehemu kusachi au kutafuta Mambo yanayotengua Udhu Mukaweka tu. Kama kwenda chooni. Kukojoa. Usingizi Mnono. kujamba. Nk. Lakini Hamjaweka Ngamia na hili ni moja wapo mambo yanotengua  Udhu. Kwa hiyo nilikua Naomba tu Munifahamishe Kuhusu Huyu Ngamia Kwa ushahidi wa Hadithi kwa sababu watu wengi sana halijui Jambo hili.



JIBU

Wa Aleykum Sallaam WarahmatulLaah  Wabarakatuh

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.


Naam katika suala hilo zipo Hadiyth zinazozungumzia ambazo zipo wazi. Hadiyth zenyewe ni:

Jaabir bin Samurah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kuwa alikuja mtu akamuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Je, tutawadhe kwa kula nyama ya mbuzi?” Akasema: “Ukitaka tawadha, na ukitaka usitawadhe”. Akauliza: “Je, tutawadhe kwa nyama ya ngamia (yaani kwa kula)?” Akasema: “Ndio, tawadheni kwa nyama ya ngamia” [Muslim na Ibn Maajah].


Imepokewa na Al-Baraa’ bin ‘Aazib (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Tawadheni kwa nyama ya ngamia, wala msitawadhe kwa nyama ya mbuzi” [Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah]

Hii ya kutawadha baada ya kula nyama ya ngamia ndio rai iliyo sahihi zaidi kwa kila hali. Kwa ajili hiyo amesema Imaam an-Nawawiy katika Sharh yake ya Swahiyh Muslim: “Na madhehebu haya ndio yenye dalili yenye nguvu zaidi japokuwa jamhuri ya ‘Ulamaa wanakwenda kinyume chake.”


Ama kuhusu nini hekima ya kutawadha baada ya kula nyama ya ngamia Hadiyth hazikutaja hilo. Kwa hiyo, Mjuzi wa hikma hiyo ni Allaah ('Azza wa Jalla)  Peke Yake nasi tunahitajika tuwe ni wenye kufuata. Kwa kufanya hivyo ni dalili ya Iymaan nzuri ya Muislamu.


Na Allaah Anajua zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Mume kunyonya maziwa ya mkewe inafaa...?

Swali Mume kunyonya maziwa (matiti) ya mkewe inafaa...? Jibu Hakuna Uharamu wa Mume  kunyonya matiti ya mke wake.  Allaah(Subhaana wa Taala) Anasema kwamba:  ((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ وَاعْلَمُواْ أَنَّكُم مُّلاَقُوهُ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ)) ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Allaah , na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wape bishara njema Waumini)) [2:223] Kwahiyo mwanamke anayo ruhusa ya kumchezea mkewe sehemu yoyote ya mwili wake pamoja na kunyonya maziwa ya mkewe isipokuwa tu Kufanya naye jimai kwa sehemu ya nyuma (liwati). Aayah hii:  “ Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. “   imeteremka kuhusu Mayahudi waliokuwa wakisema kuwa mwanaume akimuingilia mke wake kupitia upande wa nyuma basi anazaliwa mtoto akiwa ana makengeza. Ndipo i

Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye Muziki na Vinanda

Swali Inafaa Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye  Muziki na Vinanda Jibu  Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu hukumu ya muziki inayotiwa katika Nashiyd na Qaswiydah. Muziki na utumiaji wa ala za muziki ni haramu katika Dini yetu hii, Uislamu. Zifuatazo ni dalili kuhusu hilo:   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Kutakuwa watu katika Ummah wangu watakao halalisha uzinzi, uvaaji wa Hariri, pombe (unywaji) na ma’aazif (ala za muziki) ” (al-Bukhaariy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Mwisho wa zama (dunia) kutakuwa na maporomoko ya ardhi, mawe kutoka mbinguni na kugeuza kwa wanyama, wakati ambapo ala za muziki na waimbaji wanawake watakapoenea na pombe kuruhusiwa ” (atw-Twabaraniy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Watu katika ummah wangu watakunywa pombe, kuiita kwa jina jingine. Watatiwa furaha kwa uchezaji wa ala za muziki na uimbaji wa wanawake (watakao

Hukumu ya Mke kutoka nyumbani bila Ruksa ya mumewe

Naam shukrani kwa swali lako kuhusu mkeo kutoka bila ya ruhusa yako kwenda katika mishuari zake. Matatizo haya hutokea mara nyingi kwa mke kutokuwa na ufahamu na ujuzi wa Dini ya Kiislamu. Au mara nyingine huwa kweli ana elimu lakini hushindwa kufuata kimatendo kwa sababu moja au nyingine. Au huenda akawa na elimu, lakini akakosa Dini. Kwa ajili hiyo Imaam al-Bukhaariy, ana mlango katika  Swahiyh  yake wenye kichwa cha habari, “ Elimu Kabla Ya ‘Amali ”. Hata hivyo, huenda mtu akawa na elimu lakini akawa hana ‘amali kwa sababu ya kutokuwa na ikhlaasw.   Ni juu ya mke kumtii mumewe katika mambo yasiyo ya maasi, kwani hakuna utiifu katika maasiya. Ikiwa mume hakutoa ruhusa mbali na kuwa yu mbali na mkewe ni wajibu wa mke kutii amri hiyo. Hata hivyo, haifai kwa mume kuweka vikwazo vya kupita kiasi,  kama kumzuia kwenda kwa wazazi wake na mahali ambapo anaweza kupata elimu ya Kidini. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “ Wakikutiini, basi msiwatafutie njia ” (an-Nisaa’ [4]: 34). Hii