Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Maamkizi ya Kiislaam - Maamkizi ya Peponi

Maamkizi ya Kiislamu  yatakayokuwa maamkizi ya Peponi kwa dalili zifuatazo:  Kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

إِنَّ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ الْيَوْمَ فِي شُغُلٍ فَاكِهُونَ ﴿٥٥﴾
Hakika watu wa Jannah leo wamo katika kushughulika wakifurahi.

هُمْ وَأَزْوَاجُهُمْ فِي ظِلَالٍ عَلَى الْأَرَائِكِ مُتَّكِئُونَ ﴿٥٦﴾
Wao na wake zao, wakiwa katika vivuli, juu ya makochi ya fakhari wakiegemea.

لَهُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ ﴿٥٧﴾
Watapata humo kila aina ya matunda, na watapata wanavyoomba.

سَلَامٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ ﴿٥٨﴾
 “Salaamun!” Kauli kutoka kwa Rabb Mwenye kurehemu. [Yaasiyn: 55-58]

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) pindi Waumini wakishaingizwa Peponi watapokelewa na Walinzi wake wakitoa maamkizi ya Kiislamu:


وَسِيقَ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ إِلَى الْجَنَّةِ زُمَرًا ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوهَا وَفُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا سَلَامٌ عَلَيْكُمْ طِبْتُمْ فَادْخُلُوهَا خَالِدِينَ﴿٧٣﴾
Na wataendeshwa wale waliomcha Rabb wao kuelekea Jannah makundi-makundi, mpaka watakapoifikia na ikafunguliwa milango yake, na watasema walinzi wake: “Salaamun ‘Alaykum! Amani iwe juu yenu furahini na iingieni ni wenye kudumu.” [Az-Zumar: 73]

Vile vile Malaika watakapoingia kupitia milangoni ya Peponi kwa waja wema maamkizi ni hayo hayo ya Salaamun 'Alaykum:
الَّذِينَ يُوفُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَلَا يَنقُضُونَ الْمِيثَاقَ ﴿٢٠﴾
Ambao wanatimiza ahadi ya Allaah, na wala hawavunji fungamano

وَالَّذِينَ يَصِلُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ وَيَخَافُونَ سُوءَ الْحِسَابِ ﴿٢١﴾
Na ambao wanaunga yale Aliyoamrisha Allaah kuungwa na wanamkhofu Rabb wao, na wanakhofu hesabu mbaya

وَالَّذِينَ صَبَرُوا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِمْ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً وَيَدْرَءُونَ بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عُقْبَى الدَّارِ ﴿٢٢﴾
Na ambao wamesubiri kutaka Wajihi wa Rabb wao, na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa katika yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri, na wanaepusha ovu kwa zuri, hao watapata hatima njema ya makazi ya Aakhirah.

جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا وَمَن صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ يَدْخُلُونَ عَلَيْهِم مِّن كُلِّ بَابٍ﴿٢٣﴾
Jannaat za kudumu milele wataingia pamoja na waliotengenea miongoni mwa baba zao na wake zao na dhuria zao. Na Malaika wanawaingilia katika kila milango.

سَلَامٌ عَلَيْكُم بِمَا صَبَرْتُمْ ۚ فَنِعْمَ عُقْبَى الدَّارِ ﴿٢٤﴾
 “Salaamun ‘Alaykum! (Amani iwe juu yenu) kwa yale mliyosubiri.” Basi uzuri ulioje hatima njema ya makazi ya Aakhirah. [Ar-Ra'ad: 20-24]

Pia uhai na mwisho wa mwana Aadm umegusia maamkizi haya matukufu. Malaika wanapowatoa roho waja wema huwatoa huku wakiwapa maamkizi haya ya Assalaamu 'Alaykum:

الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٣٢﴾
Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema watasema: “Salaamun ‘Alaykum, (amani iwe juu yenu) ingieni Jannah kwa yale mliyokuwa mkitenda.” [An-Nahl: 32]

Hata Manabii katika uhai wao wa mwanzo na mwisho yamethibiti maamkizi ya Kiislamu kama Nabiy Yahyaa ('Alayhis-Salaam) alipoambiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

يَا يَحْيَىٰ خُذِ الْكِتَابَ بِقُوَّةٍ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا ﴿١٢﴾
 “Ee Yahyaa!  Chukua Kitabu kwa nguvu.” Na Tukampa hikma angali mtoto.

وَحَنَانًا مِّن لَّدُنَّا وَزَكَاةً ۖ وَكَانَ تَقِيًّا ﴿١٣﴾
Na mwenye upole na huruma kutoka Kwetu, na mwenye utakaso, na akawa mwenye taqwa.

وَبَرًّا بِوَالِدَيْهِ وَلَمْ يَكُن جَبَّارًا عَصِيًّا ﴿١٤﴾
Na mtiifu mno kwa wazazi wake wawili, na wala hakuwa jabari wala asi.

وَسَلَامٌ عَلَيْهِ يَوْمَ وُلِدَ وَيَوْمَ يَمُوتُ وَيَوْمَ يُبْعَثُ حَيًّا ﴿١٥﴾
Na (Salaamun ‘alayhi) amani iwe juu yake siku aliyozaliwa, na siku atakayokufa na siku atakayofufuliwa hai. [Maryam: 12-15].

Nabiy 'Iysaa ('Alyahis-Saalam) alipozungumza akiwa mtoto mchanga:

قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّـهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا ﴿٣٠﴾
 (Mtoto) Akasema: “Hakika mimi ni mja wa Allaah; Amenipa Kitabu (Injiyl) na Amenijaalia kuwa Nabiy.”

وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا ﴿٣١﴾
 “Na Amenijaalia kuwa mwenye kubarikiwa popote nitakapokuweko, na Ameniusia Swalaah na Zakaah madamu niko hai.”

وَبَرًّا بِوَالِدَتِي وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيًّا ﴿٣٢﴾
 “Na niwe mtiifu kwa mama yangu na wala Hakunijaalia kuwa jabari, muovu.”

وَالسَّلَامُ عَلَيَّ يَوْمَ وُلِدتُّ وَيَوْمَ أَمُوتُ وَيَوْمَ أُبْعَثُ حَيًّا ﴿٣٣﴾
 “Na amani iwe juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayokufa na siku nitakayofufuliwa hai.”[Maryam: 30-33]

Waja wengine ambao watakaokuwa baina ya Jannah na Moto kwa sababu amali zao zitakuwa sawa sawa katika mizani zitakapopimwa.  Hawatokuweko Motoni wala Peponi, bali watakuwa katika mnyanyuko. Hapo watazungzuma na watu wa Peponi na maamkizi yao yatakuwa ni ya Kiislamu:

وَبَيْنَهُمَا حِجَابٌ ۚ وَعَلَى الْأَعْرَافِ رِجَالٌ يَعْرِفُونَ كُلًّا بِسِيمَاهُمْ ۚ وَنَادَوْا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَن سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۚ لَمْ يَدْخُلُوهَا وَهُمْ يَطْمَعُونَ ﴿٤٦﴾
Na baina yao ni kizuizi. Na kwenye Al-A’raaf (ukuta wa mwinuko) patakuweko watu wanaowatambua wote kwa alama zao. Na watawaita watu wa Jannah: “Salaamun ‘Alaykum!”  Hawakuingia humo lakini huku wao wanatumaini. [Al-A'raaf: 46]

Ni Ahadi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuwa wakaazi wa Peponi watapata kila aina ya mazuri na wanachokitamani na katika sifa mojawapo ya Jannah ni kwamba hakuna watakalosikia baya ila maneno mema tu kama hayo maamkizi ya kiislamu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ ﴿١٠﴾
Na waliotangulia mbele, watatangulia mbele.
أُولَـٰئِكَ الْمُقَرَّبُونَ ﴿١١﴾
Hao ndio watakaokurubishwa.
فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿١٢﴾
Katika Jannaat za taanisi.

ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ ﴿١٣﴾
Kundi kubwa katika wa awali.

وَقَلِيلٌ مِّنَ الْآخِرِينَ ﴿١٤﴾
Na wachache katika wa mwishoni.

عَلَىٰ سُرُرٍ مَّوْضُونَةٍ ﴿١٥﴾
 (Watakuwa) Juu ya makochi ya fakhari yaliyotariziwa na kutonewa vito vya thamani kwa ustadi wa hali ya juu.

مُّتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ ﴿١٦﴾
Wakiegemea juu yake wakikabiliana.

يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ ﴿١٧﴾
Watazungukiwa na vijana wenye kudumu.

بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ ﴿١٨﴾
Kwa bilauri na mabirika na vikombe vya mvinyo kutoka chemchemu inayobubujika.

لَّا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنزِفُونَ ﴿١٩﴾
Hawatoumizwa vichwa kwavyo na wala hawatoleweshwa.

وَفَاكِهَةٍ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ ﴿٢٠﴾
Na matunda watakayopendelea.

وَلَحْمِ طَيْرٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ ﴿٢١﴾
Na nyama za ndege katika watakazozitamani.

وَحُورٌ عِينٌ ﴿٢٢﴾
Na mahuwr, wanawake wazuri wa Jannah wenye macho ya kupendeza.

كَأَمْثَالِ اللُّؤْلُؤِ الْمَكْنُونِ ﴿٢٣﴾
Kama mfano wa lulu zilizohifadhiwa.

جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٢٤﴾
Jazaa kwa yale waliyokuwa wakitenda.

لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا ﴿٢٥﴾
Hawatosikia humo upuuzi na wala yanayosababisha dhambi.

إِلَّا قِيلًا سَلَامًا سَلَامًا ﴿٢٦﴾
Isipokuwa itasemwa: “Salama, salama!”  [Al-Waaqi'ah: 10-26].

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Mume kunyonya maziwa ya mkewe inafaa...?

Swali Mume kunyonya maziwa (matiti) ya mkewe inafaa...? Jibu Hakuna Uharamu wa Mume  kunyonya matiti ya mke wake.  Allaah(Subhaana wa Taala) Anasema kwamba:  ((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ وَاعْلَمُواْ أَنَّكُم مُّلاَقُوهُ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ)) ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Allaah , na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wape bishara njema Waumini)) [2:223] Kwahiyo mwanamke anayo ruhusa ya kumchezea mkewe sehemu yoyote ya mwili wake pamoja na kunyonya maziwa ya mkewe isipokuwa tu Kufanya naye jimai kwa sehemu ya nyuma (liwati). Aayah hii:  “ Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. “   imeteremka kuhusu Mayahudi waliokuwa wakisema kuwa mwanaume akimuingilia mke wake kupitia upande wa nyuma basi anazaliwa mtoto akiwa ana makengeza. Ndipo i

Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye Muziki na Vinanda

Swali Inafaa Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye  Muziki na Vinanda Jibu  Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu hukumu ya muziki inayotiwa katika Nashiyd na Qaswiydah. Muziki na utumiaji wa ala za muziki ni haramu katika Dini yetu hii, Uislamu. Zifuatazo ni dalili kuhusu hilo:   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Kutakuwa watu katika Ummah wangu watakao halalisha uzinzi, uvaaji wa Hariri, pombe (unywaji) na ma’aazif (ala za muziki) ” (al-Bukhaariy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Mwisho wa zama (dunia) kutakuwa na maporomoko ya ardhi, mawe kutoka mbinguni na kugeuza kwa wanyama, wakati ambapo ala za muziki na waimbaji wanawake watakapoenea na pombe kuruhusiwa ” (atw-Twabaraniy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Watu katika ummah wangu watakunywa pombe, kuiita kwa jina jingine. Watatiwa furaha kwa uchezaji wa ala za muziki na uimbaji wa wanawake (watakao

Hukumu ya Mke kutoka nyumbani bila Ruksa ya mumewe

Naam shukrani kwa swali lako kuhusu mkeo kutoka bila ya ruhusa yako kwenda katika mishuari zake. Matatizo haya hutokea mara nyingi kwa mke kutokuwa na ufahamu na ujuzi wa Dini ya Kiislamu. Au mara nyingine huwa kweli ana elimu lakini hushindwa kufuata kimatendo kwa sababu moja au nyingine. Au huenda akawa na elimu, lakini akakosa Dini. Kwa ajili hiyo Imaam al-Bukhaariy, ana mlango katika  Swahiyh  yake wenye kichwa cha habari, “ Elimu Kabla Ya ‘Amali ”. Hata hivyo, huenda mtu akawa na elimu lakini akawa hana ‘amali kwa sababu ya kutokuwa na ikhlaasw.   Ni juu ya mke kumtii mumewe katika mambo yasiyo ya maasi, kwani hakuna utiifu katika maasiya. Ikiwa mume hakutoa ruhusa mbali na kuwa yu mbali na mkewe ni wajibu wa mke kutii amri hiyo. Hata hivyo, haifai kwa mume kuweka vikwazo vya kupita kiasi,  kama kumzuia kwenda kwa wazazi wake na mahali ambapo anaweza kupata elimu ya Kidini. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “ Wakikutiini, basi msiwatafutie njia ” (an-Nisaa’ [4]: 34). Hii