Kuweka rasta ni katika kuwaiga makafiri na si katika mila zetu za Kiislam. Uislamu unachunga nadhafa na usafi na pia mienendo yotekama tulivyofundishwa na Mtume wetu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Na yeye ndiye aliyetukataza tusijifananishe au kuwaiga wasiokuwa Waislam.
Kuhusu kujifananisha na makafiri Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
Kuhusu kujifananisha na makafiri Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((...وَمَنْ تَشَبَّهَ بِقَوْمٍ فَهُوَ مِنْهُمْ))
((Atakayejifananisha na watu, basi yeye ni miongoni mwao)) Abu Daawuud na Ahmad.
Isitoshe hali hii inakhalifu Fitwrah (Maumbile ya asli ya mwanaadam ambayo ni Uislam).
Hivyo, kuweka rasta ni jambo lisilo la Kiislam na halifai, na swali la kuwauliza wafanyao hivyo, wanafanya kwa malengo yepi? Kwa mafunzo ya nani? Kwa faida gani? Ikiwa pia kavutiwa kwa kuwaona hao ambao sehemu ya dini yao ni kuvuta bangi, basi hakika atakuwa mtu huyo hajitambui na hajui malengo yake hapa duniani na kwa sababu malengo ya wmanaadam hapa ulimwenguni ni kumuabudu Allaah na hakupatikani hilo isipokuwa mtu kuwa Muislam na kufuata mafunzo yake yote bila kuacha mengine.
Tunamuomba Allaah Awaongoze Waislam na Awaruzuku mapenzi ya kuipenda dini yao na kuifuata na kuacha kufuata mila na tamaduni zisizo za Kiislam.
Na Allaah Anajua zaidi
Maoni