Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Nchi ya Kiislamu kwa mujibu wa Ibn Baaz

Swali: Miji mingi ya Kiislamu ina mambo ya kishirki na wanawaabudu majengo ya waja wema. Je, miji hii inaitwa kuwa ni ya “Kiislamu” au hapana?

Jibu: Inategemea. Ikiwa nembo za kikafiri ndio zilizoenea kwa wingi zaidi basi ni miji ya kikafiri. Ikiwa nembo za Kiislamu ndio zilizo kwa wingi basi hiyo ni miji ya Kiislamu. Kinachozingatiwa ni kile kilichoenea na kushinda zaidi.

Swali: Wanaswali, wanafunga na kuna misikiti.

Jibu: Kunatazamwa kile kilichoea zaidi. Nchi ina hukumu kutegemea kile kilichoenea zaidi.

Swali: Wakazi wengi ni waislamu, jina ni la Kiislamu.

Jibu: Ikiwa chenye kuonekana zaidi ni jina la Uislamu, wema na mengine katika nembo za Uislamu basi ni nchi ya Kiislamu japokuwa mtawala atakuwa kafiri.

Swali: Nchi itakuwa ya Kiislamu?

Jibu: Ndio, ndio.


Rejea Kitaab Sharh Buluugh-il-Maraam (2)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Mume kunyonya maziwa ya mkewe inafaa...?

Swali Mume kunyonya maziwa (matiti) ya mkewe inafaa...? Jibu Hakuna Uharamu wa Mume  kunyonya matiti ya mke wake.  Allaah(Subhaana wa Taala) Anasema kwamba:  ((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ وَاعْلَمُواْ أَنَّكُم مُّلاَقُوهُ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ)) ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Allaah , na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wape bishara njema Waumini)) [2:223] Kwahiyo mwanamke anayo ruhusa ya kumchezea mkewe sehemu yoyote ya mwili wake pamoja na kunyonya maziwa ya mkewe isipokuwa tu Kufanya naye jimai kwa sehemu ya nyuma (liwati). Aayah hii:  “ Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. “   imeteremka kuhusu Mayahudi waliokuwa wakisema kuwa mwanaume akimuingilia mke wake kupitia upande wa nyuma basi anazaliwa mtoto akiwa ana makengeza. Ndipo i

Allaah ni nani?

                                      MTAMBUE  ALLAAH (SUBHAANA WA TAALA) Allaah ni nani? Allaah ni jina sahihi linalotumika kwa muabudiwa wa haki ambaye Yuko Mwenyewe kwa dhati Yake Mwenye Majina bora Matukufu na Sifa zisizo na shaka. Allaah ni Mmoja na Hana mfano Wake. Hana mtoto, mshirika wala mfano Wake. Yeye Ndiye Muumbaji pekee na Msimamizi wa ulimwengu. Kila kiumbe kinashuhudia Upweke Wake, Ukuu na Rubuubiyyah, na Utukufu na Majina ya kipekee. Uwepo Wake haufanani na uwepo wa kawaida. Hayuko ndani ya kitu chochote, wala hakiingii kitu chochote Kwake. لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ  ۖ  وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١١﴾   Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.  [Ash-Shuwraa: 11] Yeye ni Mmoja, Pekee, Asiyegawanyika. Yeye ni Rabb (Baadhi hufasiri neno ‘Rabb’ kwa ‘Mlezi’, maana ya ‘Rabb’ iko mbali kimaana zaidi ya kubinywa katika neno moja kama ‘Mlezi’). Rabb, ina maana, miongoni mwa maana nyengine, Muumbaji, Mpaji, Mt

Kupiga Mswaki Kwa Kutumia Dawa (Toothpaste) Kunabatilisha Swawm?

SWALI Swali langu ni kama linavojieleza hapo juu kwenye kichwa cha hahari kuhusu kupiga mswaki kwa kutumia dawa ya colgate au dawa yeyote ile,kusema kweli hili suala limeulizwa na watu wengi sana na nyinyi mashehe zetu munalipeleka kwenye category ya kitu kinachobatilisha swaum, kwa maana hiyo hili suala halipo kabisa kwenye category hiyo, sasa tunakuombeni mtujibu hili tu ili tujue inafaa au laa. Wabillahi Taufik, Massalaam. JIBU Tunashukuru kwa Swali lako kuhusu kutumia dawa ya meno katika Swawm. Hakuna makatazo ya kutumia dawa ya meno wakati unapiga mswaki ukiwa kwenye Swawm, ingawa kujiepusha kuitumia wakati wa Swawm ni bora ili usije kuimeza wakati unaitumia.  Na vizuri  zaidi kutumia miswaak aliyokuwa akitumia Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam). Lakini ikiwa haikupatikana, na kuna haja ya kutumia dawa, basi hakuna neno kusafisha meno kwa dawa ya meno.  Na kufanya h