Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Sababu za Kuwa na Miezi Mitukufu

SWALI

nilikuwa na masuala yafuatayo.
katika kuran tukufu suratul tawbah aya 35 kumetajwa kuhusu miezi mitukufu nayo ni 4,dhul qaidah(huu uloanza leo),dhul hijjah,muharam na rajab. sualalangu,nataka kujua    a)jee kuna kisa gani kulitokea mpaka ikawa mitukufu hiyo miezi.b) kuna ibada za sunna za kufunga ktk miezi hii,jee zikoje duas za kuomba n.k
shukrani sana.



JIBU



Miezi mitukufu ilijulikana kuwa ni mitukufu tokea zama za ujaahiliyyah (Kabla ya Uislamu):

 عن أبي بَكْرَةَ رضي الله عنه عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أنه قَالَ:  ((إن الزَّمَانَ قَدْ اسْتَدَارَ كَهَيْئَتِهِ يَوْمَ خَلَقَ اللَّهُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ السَّنَةُ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ثَلاثٌ مُتَوَالِيَاتٌ ذُو الْقَعْدَةِ وَذُو الْحِجَّةِ وَالْمُحَرَّمُ وَرَجَبُ مُضَرَ الَّذِي بَيْنَ جُمَادَى وَشَعْبَانَ))
Imepokelewa kutoka kwa Abu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mgawano wa zama umerudi katika hali yake ya asili siku Allaah Alipoumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi kumi na mbili; minne miongoni ya hiyo ni mitukufu, mitatu inafuatana pamoja; Dhul-Qa'adah, Dhul-Hijjah na Muharram, mwengine ni Rajab wa (kabila la) Mudhwarr ambao uko baina ya Jumaadaa na Sha'baan))  [Al-Bukhaariy na Muslim]

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefananua katika Hadiyth hiyo  kwamba ‘Rajab ya Mudhwarr’ ni kwa ajili ya kuthibitisha kauli ya kabila la Mudhwarr wanayosema kwamba Rajab ni mwezi baina ya Jumaadah na Sha’baan na sio kama walivyodhani kabila la Rabiy’ah kwamba uko baina ya Sha’baan na Shawwaal ambao ni Ramadhwaan katika kalenda ya sasa.

Miezi mitatu katika hiyo inafuatana ili iwezekane kutekelezwa fardhi ya Hajj kwa wepesi.

Dhul-Qa’adah: Mwezi wa kabla ya Hajj umefanywa mtukufu kwa sababu watu walijizuia kupigana katika mwezi huo.

Dhul-Hijjah: Umefanywa mtukufu kwa sababu fardhi na taratibu za Hajj zinatekelezwa na kukamilishwa humo.

Muharram: Unafuata baada ya Hajj, umefanywa mtukufu ili watu waweze kurudi makwao kwa usalama baada ya kutekeleza Hajj.

Rajab: Uko katikati ya mwaka, umefanywa mtukufu ili watu waliokuwa wanakuja kutoka pande za mbali za bara la Arabuni waweze kufanya ‘Umrah na kutembelea Al-Ka’bah kisha warudi makwao kwa usalama.  [Tafsiyr Ibni Kathiyr]
  
Na Allaah Anajua zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Mume kunyonya maziwa ya mkewe inafaa...?

Swali Mume kunyonya maziwa (matiti) ya mkewe inafaa...? Jibu Hakuna Uharamu wa Mume  kunyonya matiti ya mke wake.  Allaah(Subhaana wa Taala) Anasema kwamba:  ((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ وَاعْلَمُواْ أَنَّكُم مُّلاَقُوهُ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ)) ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Allaah , na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wape bishara njema Waumini)) [2:223] Kwahiyo mwanamke anayo ruhusa ya kumchezea mkewe sehemu yoyote ya mwili wake pamoja na kunyonya maziwa ya mkewe isipokuwa tu Kufanya naye jimai kwa sehemu ya nyuma (liwati). Aayah hii:  “ Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. “   imeteremka kuhusu Mayahudi waliokuwa wakisema kuwa mwanaume akimuingilia mke wake kupitia upande wa nyuma basi anazaliwa mtoto akiwa ana makengeza. Ndipo i

Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye Muziki na Vinanda

Swali Inafaa Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye  Muziki na Vinanda Jibu  Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu hukumu ya muziki inayotiwa katika Nashiyd na Qaswiydah. Muziki na utumiaji wa ala za muziki ni haramu katika Dini yetu hii, Uislamu. Zifuatazo ni dalili kuhusu hilo:   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Kutakuwa watu katika Ummah wangu watakao halalisha uzinzi, uvaaji wa Hariri, pombe (unywaji) na ma’aazif (ala za muziki) ” (al-Bukhaariy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Mwisho wa zama (dunia) kutakuwa na maporomoko ya ardhi, mawe kutoka mbinguni na kugeuza kwa wanyama, wakati ambapo ala za muziki na waimbaji wanawake watakapoenea na pombe kuruhusiwa ” (atw-Twabaraniy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Watu katika ummah wangu watakunywa pombe, kuiita kwa jina jingine. Watatiwa furaha kwa uchezaji wa ala za muziki na uimbaji wa wanawake (watakao

Hukumu ya Mke kutoka nyumbani bila Ruksa ya mumewe

Naam shukrani kwa swali lako kuhusu mkeo kutoka bila ya ruhusa yako kwenda katika mishuari zake. Matatizo haya hutokea mara nyingi kwa mke kutokuwa na ufahamu na ujuzi wa Dini ya Kiislamu. Au mara nyingine huwa kweli ana elimu lakini hushindwa kufuata kimatendo kwa sababu moja au nyingine. Au huenda akawa na elimu, lakini akakosa Dini. Kwa ajili hiyo Imaam al-Bukhaariy, ana mlango katika  Swahiyh  yake wenye kichwa cha habari, “ Elimu Kabla Ya ‘Amali ”. Hata hivyo, huenda mtu akawa na elimu lakini akawa hana ‘amali kwa sababu ya kutokuwa na ikhlaasw.   Ni juu ya mke kumtii mumewe katika mambo yasiyo ya maasi, kwani hakuna utiifu katika maasiya. Ikiwa mume hakutoa ruhusa mbali na kuwa yu mbali na mkewe ni wajibu wa mke kutii amri hiyo. Hata hivyo, haifai kwa mume kuweka vikwazo vya kupita kiasi,  kama kumzuia kwenda kwa wazazi wake na mahali ambapo anaweza kupata elimu ya Kidini. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “ Wakikutiini, basi msiwatafutie njia ” (an-Nisaa’ [4]: 34). Hii