Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Unachotakiwa kufanya pindi imamu anapozidisha Rak´ah

Swali


Nimekusikia katika moja katika Khutbah za ijumaa ukisema kwamba ni wajibu kwa mswaliji asimfuate imamu pindi atapozidisha Rak´ah katika swalah yake ya faradhi kama kwa mfano akizidisha Rak´ah ya tano. Ni vipi mswaliji atamzindua imamu? Naomba kuwekewa wazi. Imamu asiporudi na akaendelea na swalah yake katika Rak´ah ya tano mswaliji afanye nini? Je, asimame kumfuata imamu au aendelee kukaa kwake chini?



Jibu


Kumzindua imamu ni jambo limebainishwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:
“Wanaume wamsabihi Allaah na wanawake wapige makofi.”
Wanaume waseme:
سبحان الله
“Allaah ametakasika.”
Wakati fulani imamu anaposimama katika Rak´ah ya tano katika swalah yenye Rak´ah nne anaambiwa hivo lakini hata hivyo imamu huyu anaendelea. Katika hali hii mswaliji afanye nini? Maamuma akae chini na wala asimfuate imamu. Imamu atapoleta salamu ndipo nawe utoe salamu. Hilo ni kwa sababu baadhi ya imamu wanasimama katika Rak´ah ya tano kwa sababu wamesahau kusoma al-Faatihah katika Rak´ah moja wapo. 


Wanaposahau kusoma al-Faatihah katika Rak´ah moja wapo Rak´ah ile inafutika na anasimama kuswali Rak´ah nyingine ichukue nafasi yake. Kwa hivyo matokeo yake wanasimama kuswali Rak´ah ya tano badala ya ile ya Rak´ah ambayo alisahau kusoma al-Faatihah. Kwa hiyo swalah ya imamu huyu inakuwa sio batili. Kwa sababu ameswali Rak´ah ya tano kwa sababu ya kukamilisha swalah yake ambayo imepungua kwa sababu ya kuacha nguzo miongoni mwa nguzo.

Ama tutapojua kuwa imamu amesimama katika Rak´ah ya tano au katika Rak´ah yoyote ya ziada, basi tunatakiwa kunuia kutengana naye na kutoa salamu kivyetu na kumwacha. 


Kwa mfano anaswali Fajr na tukatambua kuwa imamu amesoma al-Faatihah vilivyo, Rukuu´ kikamilifu, Sujuud kikamilifu, kuinuka kutoka katika Rukuu´ kikamilifu, kikao kamilifu na Tashahhud ya mwisho kikamilifu na tukajua kuwa amesoma ndani yake, tutapoyakinisha kuwa amesimama katika Rak´ah ya ziada basi hatumfuati. 


Badala yake tunakaa na kutoa salamu. Ama midhali hatuna yakini basi tunatakiwa kukaa chini. Lakini tunamsubiri ili tuweze kutoa salamu pamoja naye.



Rejea Kitaab al-Liqaa' ash-Shahriy (50) 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Mume kunyonya maziwa ya mkewe inafaa...?

Swali Mume kunyonya maziwa (matiti) ya mkewe inafaa...? Jibu Hakuna Uharamu wa Mume  kunyonya matiti ya mke wake.  Allaah(Subhaana wa Taala) Anasema kwamba:  ((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ وَاعْلَمُواْ أَنَّكُم مُّلاَقُوهُ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ)) ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Allaah , na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wape bishara njema Waumini)) [2:223] Kwahiyo mwanamke anayo ruhusa ya kumchezea mkewe sehemu yoyote ya mwili wake pamoja na kunyonya maziwa ya mkewe isipokuwa tu Kufanya naye jimai kwa sehemu ya nyuma (liwati). Aayah hii:  “ Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. “   imeteremka kuhusu Mayahudi waliokuwa wakisema kuwa mwanaume akimuingilia mke wake kupitia upande wa nyuma basi anazaliwa mtoto akiwa ana makengeza. Ndipo i

Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye Muziki na Vinanda

Swali Inafaa Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye  Muziki na Vinanda Jibu  Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu hukumu ya muziki inayotiwa katika Nashiyd na Qaswiydah. Muziki na utumiaji wa ala za muziki ni haramu katika Dini yetu hii, Uislamu. Zifuatazo ni dalili kuhusu hilo:   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Kutakuwa watu katika Ummah wangu watakao halalisha uzinzi, uvaaji wa Hariri, pombe (unywaji) na ma’aazif (ala za muziki) ” (al-Bukhaariy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Mwisho wa zama (dunia) kutakuwa na maporomoko ya ardhi, mawe kutoka mbinguni na kugeuza kwa wanyama, wakati ambapo ala za muziki na waimbaji wanawake watakapoenea na pombe kuruhusiwa ” (atw-Twabaraniy).   Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Watu katika ummah wangu watakunywa pombe, kuiita kwa jina jingine. Watatiwa furaha kwa uchezaji wa ala za muziki na uimbaji wa wanawake (watakao

Hukumu ya Mke kutoka nyumbani bila Ruksa ya mumewe

Naam shukrani kwa swali lako kuhusu mkeo kutoka bila ya ruhusa yako kwenda katika mishuari zake. Matatizo haya hutokea mara nyingi kwa mke kutokuwa na ufahamu na ujuzi wa Dini ya Kiislamu. Au mara nyingine huwa kweli ana elimu lakini hushindwa kufuata kimatendo kwa sababu moja au nyingine. Au huenda akawa na elimu, lakini akakosa Dini. Kwa ajili hiyo Imaam al-Bukhaariy, ana mlango katika  Swahiyh  yake wenye kichwa cha habari, “ Elimu Kabla Ya ‘Amali ”. Hata hivyo, huenda mtu akawa na elimu lakini akawa hana ‘amali kwa sababu ya kutokuwa na ikhlaasw.   Ni juu ya mke kumtii mumewe katika mambo yasiyo ya maasi, kwani hakuna utiifu katika maasiya. Ikiwa mume hakutoa ruhusa mbali na kuwa yu mbali na mkewe ni wajibu wa mke kutii amri hiyo. Hata hivyo, haifai kwa mume kuweka vikwazo vya kupita kiasi,  kama kumzuia kwenda kwa wazazi wake na mahali ambapo anaweza kupata elimu ya Kidini. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “ Wakikutiini, basi msiwatafutie njia ” (an-Nisaa’ [4]: 34). Hii